Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>Kasi ya Rais Magufuli watumishi waanza kujiuzulu.Fahamu zaidi hapa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
George Simbachawene amesema kasi ya Rais Dkt John Magufuli na serikali
yake tayari watumishi wameanza kuandika barua za kuomba kujiuzulu na
kutafuta kazi sehemu nyingine.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo ingawa hajataja majina ya
watumishi hao na halmashauri wanazotoka, katika kipindi cha dakika 45
kinachorushwa na ITV na kusema kuwa yeye binafsi ameshapokea barua za
watumishi watatu kutoka kwenye halmashauri ambao hawana makosa yoyote ya
kiutendaji lakini wameamua kuandika barua ya kuomba kuachia kazi hizo.
”Kasi ya Rais Dkt. Magufuli haitawaacha watumishi wazembe wameendelee
kufanya kazi kwa maana mazoea kazini hayapo ndiyo maana mimi
nimeshapokea barua ya watumishi watatu wakiomba kujiuzulu nyazifa zao na
kweli kama kuna kiongozi anaona hataweza kwenda na kasi ya Rais na
Wizara yangu ni bora aondoke mapema kabla sijatumbuliwa mimi
nitawatumbua wao”. Amesisitiza Chawene.
Aidha Waziri Simbachawene ameeleza kusikitishwa kwake na watumishi
ambao wameshindwa kuwapandisha madaraja watumishi waliopo chini yao kwa
uzembe wao jambo ambalo linawafanya watumishi kuishi kwa malalamiko na
kukosa imani na serikali yao.
”Mimi sitamvumilia afisa utumishi yeyote ambaye hatawapandisha
madaraja watumishi waliopo chini yake wakati sifa wanazo huko ni
kuharibu maisha ya watu na serikali hii haipo tayari kuvumilia watumishi
kama hao” Amesema Waziri Simbachawene
Related Posts:
Imefichuka... Unene Kupita Kiasi Chanzo cha Ugonjwa wa Kansa..!!!.Fahamu zaidi hapa.
WANASAYANSI wa Uingereza wanasema wamethibitisha kuwepo kwa uhusiano mkubwa kati ya kunenepa na aina 11 za saratani.
Watafiti wamebaini unene unasababisha saratani kadhaa ikiwemo saratani ya tumbo, ini, matiti, utumbo n… Read More
Rais Magufuli Amteua Mama Salma Kikwete Kuwa Mbunge wa Viti Maalum.Fahamu zaidi hapa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo
tarehe 01 Machi, 2017 amemteua Mhe. Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Viti
Maalum wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Salma Kikwete ni… Read More
Polisi Watinga Nyumbani kwa Gwajima....Mwenyewe Agoma Kufungua Mlango.Fahamu zaidi hapa.
Jeshi
la Polisi kwa mara nyingine jana lilizingira nyumba ya Askofu wa Kanisa
la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwa kile lilichodai kuwa lilifika
kufanya uangalizi.
Taarifa ambazo zimethibitishwa na Askofu … Read More
#BREAKING NEWS>>WATU WANAO DHANIWA NI POLISI WAVAMIA NYUMBA YA GWAJIMA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Watu
wanaodhaniwa kuwa ni polisi wamezingira Nyumba ya Askofu Mkuu wa
Makanisa ya Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima huko Salasala muda huu.
Bado haijafahamika wanatafuta nini.
Download Application ya Heb… Read More
Waziri Nape: Nitajiuzulu Uwaziri Kama Itabainika Natoka Kimapenzi na Wema Sepetu.Fahamu zaidi hapa.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema atajiuzulu
uwaziri endapo mtu atampelekea ushahidi wa kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na msanii yeyote.
Kauli
hiyo ya Nape inakuja ikiwa ni takriban … Read More
0 comments:
Post a Comment