Wednesday 11 May 2016

#YALIYOJIRI>>>>Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kaongeza siku za bure kupanda Mabasi ya Haraka.Fahamu zaidi hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea kituo cha Mabasi yaendayo haraka cha Kamata Kariakoo leo, amesema kuwa kuanzia jumatatu Mei 16, 2016 ndio nauli za mabasi ya mwendo wa haraka zitaanza kutozwa.
Pia amewaasa watumiaji wa barabara hasa watembea kwa miguu, baiskeli na maguta wasitumie barabara hizo ili kuepusha usumbufu kwa madereva wa mabasi ya mwendo wa haraka. 
Amesema ameamua kuongeza muda wa kuanza kutoza nauli hizo kwa watumiaji wa mabasi hayo kwaajili ya kuelimisha wananchi namna ya kukata tiketi na jinsi ya kuzitumia wakati wanapoingia kwenye kituo kwaajili ya kusubiri magari.

0 comments:

Post a Comment