Tuesday 10 May 2016

#YALIYOJIRI>>>>Serikali Yakata Rufaa Kwa Mara Pili Kupinga Bosi wa Zamani wa TRA na Wenzake Kufutiwa Shitaka la Kutakatisha PesaFahamu zaidi hapa.

Upande wa Jamhuri umekata rufaa kwa mara ya pili katika kesi inayowakabili Harry Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomoni katika Mahakama ya Rufaa baada ya rufaa hiyo kukataliwa katika Mahakama Kuu.

Kitilya, alikuwa Kameshina Mkuu wa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Sinare, Mkuu wa Idara ya ushirikiano na Uwekazaji Katika Benki ya Stanbic na Sioi, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic

Rufaa hiyo imekatwa na Buswalo Mganga, Mwendesha mashitaka wa Serikali (DPP) katika kesi hiyo baada ya kutoridhika na uamuzi wa Mahakama Kuu ulifanywa wiki iliyopita na Moses Mzuna, Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Mganga alitangaza kukata rufaa mara baada kushindwa pingamizi lao la kupinga kufutwa kwa shitaka la nane la utakatishaji fedha lililofutwa na Emilis Mchauru Hakimu Mkazi Kisutu.

Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kutenda makosa saba baada ya kufutwa kosa la nane na kwamba bado watuhumiwa hao wapo lumande.

Jalada la kesi hiyo lipo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kwamba kesi hiyo ilipangwa kutajwa tena tarehe 18 Mei mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment