Kiungo
kinda wa Azam FC, Farid Mussa ameanza maandalizi yake tena kujiandaa
kwenda Hispania kujiunga na timu yake ya Derportivo Tenerife ya
Hispania.
Tayari
Farid amepata matumaini mapya baada ya leo kutinga kwenye ubalozi wa
Hispania na kuanza kushughulikia kibali cha kufanya kazi nchini humo.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi amethibitisha kwamba mambo yanakwenda vizuri.
"Kuna
matumaini makubwa kwamba sasa mambo yataenda vizuri na Farid alikuwa
ubalozini kwa kuwa tayari klabu ya Tenerife imeishawasiliana na ubalozi
wa Hispania hapa nchini," alisema.
Awali kulikuwa na
hofu ya kuua kipaji chake kwa kuwa suala la kibali kilionekana kuwa
tatizo huku Farid akiendelea kukaa benchi kwa kuwa hawezi tena kuichezea
Azam FC.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment