Sunday, 30 April 2017

BAADA ya Polisi Nane Kuuawa Kinyama..Milango ya Kanisa Yavunjwa Kibiti.Fahamu zaidi hapa.

Baada ya kuwapo matukio ya mauaji walayani hapa, Kanisa Katoliki Kigango cha Jaribu/Mjawa  katika Parokia ya Kibiti Mkoa wa Pwani, limevunjwa mlango wake na watu wasiojulikana kisha kuchoma moto majoho manne ya viongozi wa kanisa hilo.
Kiongozi wa kanisa hilo, Katekista Joseph Mwilu amesema tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku.
Mwilu  amesema akiwa kwake alipigiwa simu na mweka hazina, Mastiga Elias anayeishi jirani na kanisa hilo kuwa kuna moto unaowaka kanisani hapo.
Amesema baada ya kupata taarifa hiyo amesubiri hadi asubuhi ya jana ndipo alipofika kanisani hapo na kukuta mlango umevunjwa.
Alifafanua kuwa baada ya kufika mlangoni aliona kuna karatasi iliyoachwa hapo kikiwa na maandishi yafuatayo.
“Tunatoa tahadhari, mmewaua ndugu zetu wawili siku ya Jumamosi, sisi leo tunaanza kazi, tuko 12 na hatushindwi.  Kuanzia ngazi ya kijiji, kata hata wilaya, walimu, madaktari, manesi, watendaji wa vijiji na hata taasisi zote.  Tunashukuru kwa ushirikiano wenu,” amenukuu kimemo hicho kilivyokuwa kimeandikwa.
Amesema baada ya kuingia ndani ya kanisa alibaini majoho manne ya viongozi wa kanisa hilo yalichomwa moto, mawili yakiwa yanayovaliwa na makateksta na mengine huvaliwa na watumishi wa misa.
Vilevile amesema alipoangalia kwa umakini mkubwa alibaini pia vitambaa vinne vya madhabahuni navyo vilikuwa vimechomwa moto na dirisha moja.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Onesmo Lyanga amethibitisha kwa njia ya meseji kutokea kwa tukio hilo.
“Tunafuatilia ili kupata taarifa kamili,” ulisomeka hivyo ujumbe huo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

#BREAKING NEWS>>>LOWASSA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU JINA LA MWANAYE KUWA KWENYE LIST YA VYETI FEKI.

habari inayo Gonga vichwa vya watu ni kuhusu vyeti feki kubwa zaidi ni Pale Jina la mtoto wa Lowassa kuwemo kwenye List ya wenye vyeti feki kiendo ambacho kime Mfedhehesha sana Lowassa na kusema kuwa Hata lifumbia macho hili swala la Mwanaye kuwekwa kwenye List ya vyeti feki Lowassa Nitalitolea Ufafanuzi Jina la Godfrey Ngoyai Lowassa lililopo kwenye list ya watu wenye vyeti feki Muda sio Mrefu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

TRUMP Akejeli Jaribio La Kombora La Korea Kaskazini Jana, ‘Ni Dharau’.

Rais wa Marekani, Donald Trump amekejeli jaribio la kombora la kinyuklia la Korea Kaskazini lililofanyika jana, akidai kuwa ingawa limeshindwa ni dharau kwa China.
Jana, Korea Kaskazini ilidai kufanya jaribio lake la kombora la Nyuklia ambalo Marekani ilidai kuwa lilishindwa hata kuvuka mipaka ya nchi hiyo ndani ya dakika chache tangu lilipofyatuliwa.
“Korea Kaskazini imedharau matarajio ya China na ni dharau ya hali ya juu kwa Rais [wa China], ingawa limeshindwa, jaribio la makombora la leo. Mbaya!,” Tafsiri isiyo rasmi ya Tweet ya Rais Trump.
Trump alisema kuwa angependa sana kuumaliza mgogoro wa makombora ya kinyuklia wa Korea Kaskazini kwa njia ya kidiplomasia, lakini ni vigumu sana kutumia njia hiyo.
Katika mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN) uliofanyika jana jijini New York, wajumbe walilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo zaidi vya kiuchumi na kidiplomasia.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Rais Magufuli Ahudhuria Ibada ya Jumapili Katika Makanisa Mawili Tofauti Mjini Moshi.

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Aprili 2017, ameungana na waumini wa dini ya Kikristo kusali ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi  ,Parokia ya Kristo Mfalme na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro na kuwataka waumini wa makanisa hayo na Watanzania kwa ujumla kuendeleza amani iliyopo nchini kwa kuwa ndio chachu ya Maendeleo.

Rais Magufuli amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya Tano zina lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ya taifa linalomuamini MUNGU.

'' Napenda muniamini kuwa mimi nipo kwa niaba yenu, najua huu Urais si wangu, Urais mnao ninyi mlioamuwa nitumike kama mtumishi kwa wakati huu, nawaomba sana muendelee kuniweka katika sala zenu ili kazi hii ya Urais isinipe kiburi, nikawe mtumishi wa watu'' Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewashukuru waumini wa makanisa hayo mawili na watanzania kwa ujumla kwa kusimama pamoja kuliombea Taifa amani iliyowezesha wananchi kupiga kura kwa amani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kutokana na sala zao Mwenyezi MUNGU akamuwezesha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Rais Magufuli ametoa msaada wa mifuko 100 ya Saruji kusaidia maendeleo ya kanisa Katoliki na Shilingi Milioni Moja kwa Kwaya ya Kanisa hilo ili irekodi nyimbo zake, halikadhalka katika Kanisa la KKKT, Mheshimiwa Rais ametoa mifuko 150 ya Saruji kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Kanisa hilo na Shilingi milioni Moja kwa Kwaya ya Kanisa hilo.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuunga mkono Rais Magufuli kwa Kuchangia Mifuko hamsini ya Saruji ambapo Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick amechangia mifuko hamsini ya Saruji na Shilingi laki Tano.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi ,Parokia ya Kristo Mfalme Askofu Isaac Amani amemshukuru Rais Magufuli kwa uwamuzi wa kusali kanisani hapo na kuwataka waumini wa kanisa hilo na Tanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea yeye pamoja na Serikali yake ili iweze kuwatumikia Watanzania katika kuwaletea maendeleo na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano kwa Bara la Afrika.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - KKKT, Askofu Dr Fredrick Shoo amewataka waamini wa kanisa hilo na watanzania kwa ujumla kutokuwa na hofu kwa mambo yanayofanywa na Rais hususani katika kupambana na maovu, dhuluma na ufisadi vikiwemo na badala yake Watanzania wabadilike na kujijengea mazoea ya kufanya kazi halali na kuwa waaminifu na kuwa wazalendo kwa Taifa lao.

Aidha, Askofu Shoo amemuomba Dkt Magufuli kuangalia uwezekano wa kupunguza kodi hususani kwa taasisi za kidini zinzotoa huduma za kijamii zikiwemo zile za Elimu na Afya.

Akijibu Maombi hayo Rais Dkt Magufuli amewaeleza waamini na watanzania kwa ujumla kuwa Serikali inathamini michango ya huduma za kijamii zinazotolewa na Taasisi za dini na kuahidi kuliangalia suala hilo.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU.
Moshi, Kilimanjaro.
30 Aprili, 2017.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

LIVE IBADANI GWAJIMA ATOA UFAFUNUZI WA TRENI YA UMEME NA VYETI FEKI.




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

KIKOSI CHA YANGA KINACHOIVAA MBAO FC PALE CCM KIRUMBA MWANZA.

Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Mbao FC 
1. Deogratius Munishi 
2. Hassan Kessy
3. Haji Mwinyi
4. Vicent Andrew 
5. Nadir Haroub
6. Juma Saidi 
7. Simoni Msuva 
8. Thabani Kamusoko 
9. Obrey Chirwa 
10. Amissi Tambwe 
11. Haruna Niyonzima 

Akiba
Beno Kakolanya
Oscar Joshua
Juma Abdul
Juma Mahadhi
 Emanuel Martin
Geofrey mwashuiya
Deusi Kaseke



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

JOSHUA AWANIA KUWA MWANAMICHEZO TAJIRI UINGEREZA, HAMILTON, ROONEY WANAONGOZA.

TANO BORA YA WANAMICHEZO TAJIRI UINGEREZA

Baada ya kuingiza kitita cha pauni milioni 15 kutokana na ushindi wa jana, bondia Anthony Joshua, anaonekana anaanza kujivuta kwenye listi ya wanamichezo matajiri duniani.

Joshua alimtwanga mkongwe Wladimir Klitschko katika pambano kali la ngumi za kulipwa, imemuingizia kitita cha pauni milioni 15 ambazo ni Sh bilioni 42.5.

Hata hivyo, Lewis Hamilton, anaendelea kuongoza akiwa na kitita cha zaidi ya pauni milioni 100 kwa mwaka.

Anafuatiwa na nahodha wa Man United, Wayne Rooney anayeingiza kitia cha pauni milioni 85 kwa mwaka wakati mcheza tenisi nyota zaidi wa Uingereza, Andy Murray anapata pauni milioni 60 kwa mwaka.

Kutokana na umaarufu alionao, kama Joshua atapigana pambano jingine, ana uhakika wa kupanda haraka.

Kwani pamoja na fedha za mapambano, wadhamini huongezeka kwa kasi kubwa kutokana na umaarufu wa mwanamichezo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

RAY C -Hapa Kazi Tu, Mapenzi Baadaye.

Msanii mkongwe wa muziki, Ray C, amedai kwa sasa anapambana kuhakikisha anafanya vizuri katika muziki wake.
Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri kipindi cha nyuma na wimbo ‘Mapenzi Matamu’, alikuwa kimya kwenye muziki kwa muda mrefu akijaribu kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ambazo zlimuathiri kwa kiasi kikubwa.
Akiongea  wiki hii akiwa mwenye siha njema, Ray C amedai anachokifikiria kwa sasa katika maisha yake ni muziki na siyo mapenzi.
“Mimi sina mpenzi,” alisema Ray C “Kwa sasa nafikiria kuhusu muziki wangu sitaki kujichanganya na mambo mengine. Mashabiki wangu wamenipambania kwa muda mrefu siyo kwaajili ya mpenzi wangu, wao wanataka kazi, muziki mzuri,”
Muimbaji huyo ambaye anafanya kazi chini ya Wasafi.Com ya Diamond Platnumz anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Unanimaliza’.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya albamu yake mpya.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

#BREAKING NEWS>>>Tetemeko jingine latokea Bukoba.

Reporter wa AyoTV ameripoti kutokea mtaa wa Rwamishenye manispaa ya Bukoba kwamba limetokea tetemeko. Amesema tetemeko hilo ambalo limetokea mida ya saa saba na nusu usiku huu wa kuamkia April 30, lilidumu kwa sekunde zisizozidi 15.

Mpaka sasa anazunguka kwenye mitaa mbalimbali na anachoshuhudia ni Watu mbalimbali waliotoka nje ya nyumba zao kuhofia tetemeko jingine. Hakuna madhara yoyote yaliyoripotiwa mpaka sasa lakini AyoTV na millardayo.com zinaendelea kufatilia kwa ukaribu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Saturday, 29 April 2017

#BREAKING NEWS>>>PAMBANO LA (JOSHUA VS KLITSCHKO) JOSHUA ASHINDA KWA TKO.


RAUNDI YA 1:

Raundi imeanza kwa kasi lakini baadaye kila bondia ameonekana kutegea na kumspma mwenzake
RAUNDI YA 2:
Joshua alianza kwa kasi, akatawala na kupiga kama ngumi tano nzuri, Klitshcko akajibu kama tatu na mwisho hakukuwa na mashambulizi zaidi ya kuvisiana tu
RAUNDI YA 3:
Joshua kaana raundi hii kwa kasi kubwa na kushambulia kwa ngumi za mfululizo. Hali ambayo ilionekana kumchanganya Klitchko ambaye baadaye aliweza kutulia na kuanza kujibu mashambulizi lakini hayakuwa makali kama ya Joshua.
RAUNDI YA 4:
Klitshcko kaanza na kasi ya kimondo na ngumi zake tatu zinatua usoni kwa Joshua ambaye alikuwa hajajipanga, lakini baadaye akatulia na kujibu mashambulizi vikali hali iliyomlazimu Klitshcko kuanza kukumbatia. Mwisho Joshua ndiye amefanya vizuri zaidi.
RAUNDI YA 5:
Joshua anaonekana kuanza vizuri raundi hii akishambulia lakini mwishoni mpinzani wake naye anajitahidi kutulia baada ya kuhesabiwa na mwamuzi kutokana na kuwa na hali mbaya.
RAUNDI YA 6:
Konde kali la mkono wa kulia, Joshua anakwenda chini, Klitschko ndiye anashambulia zaidi katika raundi hii, mara kadhaa Joshua analazimika kukimbia
RAUNDI YA 7:
Hii raundi inaonekana haina mwenyewe kwa kuwa kila mmoja anajaribu kushambulia lakini raundi ya 5 na 6 inaonekana kuwachosha, hawakuwa na makeke sana.
RAUNDI YA 8:
Joshua alianza vizuri na ndiye ameshambulia vizuri zaidi. Makonde mengi yanamfikia Klitshchko lakini mkongwe anapiga jab nyingi zaidi ambazo Joshua anapaswa kuwa makini
RAUNDI YA 9:
Joshua anaonekana kubadili aina ya upiganaji kwa kupiga jab nyingi lakini Klitschko bado yuko imara. Joshua anaonekana kurejea vizuri
RAUNDI YA 10:
Klitschko anaonekana kufanya vizuri anamshambulia sana na mwishoni Joshua anaonekana kuchoka.
RAUNDI YA 11:
Klitschko anaonekana kuzidiwa tokea mwanzo, Joshua anashambulia kama umeme, lakini Joshua anaonekana kama amchoka. Mwisho Klitschko anakosea, ngumi moja inaonekana kumlevya na Joshua anashambulia mfululizo na kumuangusha, Klitschko anahesabiwa na kurejea.

Joshua anamshambulia kama nyuki na kumuangusha, anainuka na kuendelea lakini anapigwa tena na mwamuzi anamuokoa Klitschko....JOSHUA AMESHINDA KWA TKO.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>
>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

#PICHA:Matukio ya pambano kati Anthony Joshua na Klitschko na kuishia Anthony Joshua kupata ushindi.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

PAMBANO LA JOSHUA DHIDI YA KLITSCHKO SASA LIKO LIVE TV1.

Pambano la ngumi za kulipwa kati ya Anthony Joshua dhidi ya Wladimir Klitschko tayari liko LIVE kupitia TV1.

Kwa sasa yameanza kuonyesha mapambano ya utangulizi.

Pambano kati ya Joshua wa Uingereza na Klitshcko raia wa Ukraine kuwania mikanda ya IBF na WBA, limekuwa likisubiriwa kwa hamu.

Mashabiki wengi wa ngumi wamepiga simu SALEHJEMBE wakiuliza kama kweli linaonyeshwa LIVE.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Italy hajulikani Alikiba wala Diamond - Hussein Machozi.

Msanii wa muziki, Hussein Machozi, amefunguka kwa kudai kuwa, hakuna msanii wa muziki kutoka Tanzania ambaye anajulikana nchini Italy.
 Aidha amedai muimbaji kutoka Kenya, Stella Mwangi ambaye anaishi nchini Norway, ndiye msanii wa Afrika Mashariki anayefanya vizuri nchini humo.
Muimbaji huyo aliyewasili nchini Tanzania wiki hii akitokea Italy, amedai muziki wa Tanzania haujafika huko na hata wasanii wanaofanya vizuri nchini kwa sasa akiwemo Diamond na Alikiba hawajulikani.

“Hapana lakini kuna mtu mmoja alishaniambia kuhusu msanii wa Kenya anaitwa Stella Mwangi wanamfahamu fahamu, siyo kivile sana kutoka East Africa,” alisema Hussein.

Aliongeza, “Bongo Fleva Italy sijawahi kuisikia kiukweli wa Mungu. Kama kuna mshikaji mmoja nilimwambia kwetu kuna msanii mkali sana anaitwa Diamond nikawa nimempa link akawa shabiki, akawapa na wengine wakawa mashabiki wa Diamond kinyama.,”

Muimbaji huyo amedai amekuja nchini kwaajili ya kuachia kazi zake mpya za muziki na baada ya hapo atarejea tena Italy kwaajili ya kuendelea na masomo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Download wimbo mpya wa Nikki Mbishi unaoitwa "Pumzisha Mwili Wako".


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa