Emmanuel Macron ameshinda Uchaguzi wa Urais wa Ufaransa. Matokeo
yanaonesha Macron amemuacha mbali mpinzani wake Bi Marine Le Pen kwa
kujinyakulia asilimia 65 ya kura. Maelfu ya wanaomuunga mkono Macron
walisherehekea katika kati mwa Paris wakipeperusha Bendera. Akiwa na
miaka 39, Macron anakuwa Rais mdogo zaidi wa kuchaguliwa kuwahi
kuiongoza ufaransa na wa kwanza kuchaguliwa kutoka nje ya vyama viwili
vikubwa.
Katika taarifa yake, amesema kwamba Ufaransa imefanikiwa kufungua
ukurasa mpya katika historia yake na kwamba alikuwa na ndoto ya kuwa
mpiga mbiu wa nchi hiyo kwa kugunduliwa upya kwa matumaini na
imani.Mshndi huyo wa nafasi ya urais ametoa hotuba yale ya kwanza akiwa
ni raisi mteule. Emmanuel Macron, amenukuliwa akisema kwamba
atahakikiksha anafanya kila linalowezekana kulipa fadhila ya uaminifu wa
wafaransa waliompa.
Wafaransa wenzangu, mlioko ndani na nje ya ufaransa, baada ya vita ya
muda mrefu vya kidemokrasia , na kuchagua kuweka imani yenu juu yangu.
Ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa heshima
kubwa.
Macron anasema ni heshima kubwa na mmenipa wajibu mkubwa wa kutekeleza,
bila kauli yoyote kwangu, natoa shukrani zangu za dhati kutoka ndani ya
moyo wangu.shukrani hizi zimfikie kila mmoja wenu, kwa kura yako na
kuniunga mkono. Sitasahau kwamwe, nitakuwa muangalifu sana na
nitahakikisha kwa nguvu zangu zote naheshimu imani yenu kwangu.
Lepen amempongeza Macron kwa njia ya simu. Na kusema kwamba chama chake
cha National Front kimepata ushindi mkubwa kwa kugawana kura, na
kufanikiwa kuigawa Ufaransa kati ya wazalendo na watawala.
Marine Le Pen aliyekuwa na matumaini ya kuikwaa nafasi ya rais wa
Ufaransa tayari amekubali kushindwa dhidi ya mpinzani wake Emmanuel
Macron .watu wa Ufaransa wamemchagua rais wa Jamhuri, na wameamua kuwa
na muendelezo . Nimempigia simu bwana Macron kumpongeza kutokana na
ushindi wake
kwasababu nina wiwa moyoni mwangu na nina itakia mema nchi
hii.Nimemtakia mafanikio mema katika changamoto zinazoikabili
Ufaransa.Ningependa kuwashukuru raia wa Ufaransa milioni kumi na mmoja ,
ambao waliamua kunipa mimi sauti zao na imani yao juu yangu, pamoja na
wanaharakati, ambao waliniunga mkono na kunipa ushirikiano wakati wote
wa kampeni,nina furaha kubwa, kwasababu ni ushindi mkubwa kwa ulaya
yote, ni ushindi kwa ulaya, ni mkubwa.
wafaransa walionesha furaha yao; ni ushindi mkubwa wa asilimia sitini na
tano , hatukulitarajia hilo, naaa, ndo hivyo, ni utawala mwingine kwa
Ufaransa. Huwezi kuamini, nina matumaini kwamba naamini atapata uungwaji
mkono katika bunge la uchaguzi mnamo mwezi june na huenda ukaleta
mabadiliko makubwa nchini. itastaajabisha.
Marina naye alisikika akisema; nimeridhika sana, ushindi huu umeiokoa
Ulaya, nastaajabia kabisa, ni suala halisi, naamini itasababisha ulaya
ijichekeche, nafikiri italeta mabadiliko makubwa , tutashuhudia
mabadiliko makubwa yakiambatana na maelekezo mapya, ni ajabu,
mastaajabu, asante.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment