Rais Magufuli alipokuwa akiongea na wafanyabiashara nchini juzi
alisema serikali sio kwamba haitaki kushirikiana na sekata binafsi na
inatambua mchango wa sekta binafsi kwa uchumi wa nchi
Wafanyabiashara kutokuwa waaminifu
Waziriwa ardhi ametaja compexity kwenye umiliki wa ardhi, amesema
kuna wafanyabiashara amabao sio waaminifu na lazima wamuone mchungu
Ametolea mfano kuna mfanyabiashara aliyenunua ardhi Tanzania hekta
132,000 na kwenda kuombea mkopo mabenki ya Uholanzi mwaka 2015 na ardhi
yenyewe haijaifanyia kazi kabisa
Mfanyabiashara huyo alishirikiana na RUBADA taasisi ya serikali
akataka kununua nyingine zaidi ya 300,000 maeneo ya Rufiji akafanye tena
hivyo
Pia amesema sekta binafsi wamekuwa na tamaa sana akatolea mfano
tenda ya kujenga hosteli za UDSM kuwa walikuwa waijenge kwa bilioni hadi
200 lakini TPBA walijenga kwa bilioni 10 tu
Sukari
Pia amezungumzia sakata la sukari kuwawafanyabiashara walikuwa
wanaficha na wakiona demand ya sukari pia imekuwa kubwa mfano kipindi
cha mfungo wanapandisha kwa makusudi
Na amedai pia aliwapa wenye viwanda vibali vya kuagiza sukari nje
kwa kjuwa wao ndio sukari ya nje inaathiri viwanda vyao lakini wenye
viwanda wakaviuza tena vibali kwa wafanyabiashara
Wafanyabiashara kuhujumu kilimo
Rais na waziri mkuu pia amezungumzia wapo wafanyabiashara wanaokuwa
wanahujumu kilimo kwa kukopa fedha kwenye benki ya kilimo ambazo
serikali ndio imekuwa ikiiwezesha lakini wamekuwa wakifanyia fedha hizo
mambo mengine kama kununua malori ya usafirishaji makontena
Alimsusia waziri mkuu wa India
Pia amesema alisusia kwenda kuweka jiwe la msingi kwenye plant ya
kufua umeme aliyoambaiwa na waziri mkuu wa India alipokuja kwa sababu
waziri mkuu huyo alimchomekea tu alipokuja na terms zao wala
hazikujulikana na hakutaka kuiweka nchi kwenye IPTL nyingine
Kuibiwa na makampuni ya madini
Pia amesema makampuni ya madini yanapaswa yaweke hisa zao soko kuu
la DSM kwa kuwa wamekuwa hawana accounts za kuzishika wala assets zozote
mkiingia kwenye dispute na fedha wanazoleta nchini ni za mshahara tu,
na wanakuwa wana declare losses kwenye statement zao na kwenye stock
exchange London hisa zao zinafanya vizuri
Ila amesema changamoto za wafanayabiashara amezisikia na
atazifanyia kazi na wakikwazwa na mtu serikalini basi wasisite kutaarifu
mawaziri wake au yeye na sio kusema serikali ni mbaya
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment