Wednesday 4 April 2018

Diamond, Samatta Waitwa Marekani Kutunukiwa Tuzo.

Mwanamuziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul maarufu Diamond Plutnumz na mwanasoka wa kimataifa, Mbwana Samattapamoja na Watanzania watatu na raia wa Marekani, wameteuliwa kutunukiwa tuzo katika tamasha lililoandaliwa na Watanzania waishio ughaibuni (Diaspora) litakalofanyika Dallas nchini Marekani.

Katika tuzo hizo atapewa  Dk Steve Meyer ambaye ni daktari bingwa katika Hospitali ya Mercy iliyopo jiji la Sioux, Marekani aliyewatibu manusura wa ajali ya wanafunzi wa Lucky Vincent.

Akizungumza na gazeti hili kutoka Dallas jana, mratibu wa tamasha hilo, Ben Kazora alisema wanampa tuzo daktari huyo kwa kutambua mchango wake katika kuokoa maisha ya watoto hao.

“Sote tunatambua namna ajali ilivyokuwa mbaya na ilivyopoteza wapendwa wetu wengi. Dk Meyer na timu yake walifanya kila njia kuokoa maisha ya watoto wale watatu walionusurika,” alisema.


“Tunampa Diamond zaidi kwa kutumia kipaji chake cha muziki kuitangaza nchi kitaifa na kimataifa, vivyo hivyo Samatta kwa kutumia kipaji chake cha kusakata kabumbu kuitangaza Tanzania,” alisema.

Kwa mujibu wa Kazora, mwingine ni mwanariadha John Akhwari ambaye mwaka 1968, alimaliza mbio katika michezo ya Olympic iliyofanyika Mexico City licha ya kuumia mguu.

Naye meya wa Dallas Texas nchini Marekani, Mike Rawlings aliwakaribisha Watanzania hao kushiriki tamasha la Tanzania Day, litakalofanyika jijini humo kwa lengo la kutangaza fursa za biashara na utalii.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment