Wednesday 18 April 2018

Yanga Leo Kupambana na Wolaitta Dicha ya Ethiopia kwa Mechi ya Marudiano.

YANGA leo inacheza mechi ya marudiano na Wolaitta Dicha ya Ethiopia katika kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho, tayari timu hiyo imepambana na kuvivuka vikwazo viwili.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, timu yake imeshapambana na baridi kali iliyopo Awassa huko Ethiopia watakapocheza mechi yao pia wamemaliza tatizo la ubutu katika safu yao ya ushambuliaji.

Yanga leo inacheza mechi ya marudiano na Dicha ugenini mjini Awassa huko Ethiopia ili kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya awali kushinda mabao 2-0 nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na Championi Jumatano, Nsajigwa alisema, hali ya hewa pekee ndiyo ilikuwa ikilalamikiwa na wachezaji wake na sasa wameahidi kupambana nayo.

Nsajigwa alisema: “Hatutaki kuifanya hali ya hewa ya baridi iwe sababu ya sisi kupoteza mchezo huu, nataka wachezaji kila mmoja kutimiza wajibu wake ndani ya uwanja ili kufanikisha ushindi katika mechi hiyo.

“Tulifika mapema kwenye mji huu kwa ajili ya wachezaji kuzoea hali ya hewa ya hapa ikiwa ni siku mbili tulizofanya mazoezi ya pamoja.

“Hadi kufikia siku ya mchezo huo tutakuwa tumefikisha saa 48, hivyo benchi letu la ufundi lina matumaini mazuri ya wachezaji wetu kuzoea hali ya hewa ya baridi tuliyoikuta hapa.


“Tayari tumefanyia marekebisho kwenye kikosi chetu baada ya mechi iliyopita tuliyocheza nyumbani ambayo ni safu ya ushambuliaji pekee ambayo ilikosa umakini katika kufunga mabao.”

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment