Monday 26 March 2018

TCRA Kutoa Hatima ya Times Fm Maojiano na Diamond Wiki Hii.

Hatima ya Kituo cha Redio Times cha jijini Dar es Salaam kilichotakiwa kuwasilisha kipindi cha mahojiano waliyoyafanya na mwanamuziki Diamond Platinumz kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ajili ya uchunguzi zaidi, itajulikana wiki hii.

Taarifa zilizoifikia MCL Digital leo Jumatatu Machi 26, 2018 zinaeleza kuwa kamati ya maudhui ya TCRA iliyokuwa ikifanya uchunguzi huo inakaribia kumaliza kazi hiyo.

Machi 22, 2018, Times ilipokea barua ya kuwataka wawasilishe kipindi hicho kilichorushwa Machi 19, 2018 na kutii agizo hilo.

Mwanamuzi Diamond alizua mjadala baada ya kuzungumzia suala la nyimbo za wasanii hao kufungiwa akimlalamikia Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kutowatendea haki wasanii.

Ofisa Mkuu Idara ya Utangazaji wa mamlaka hiyo, Andrew Kisaka ameieleza MCL Digital leo kwamba tayari kamati ya maudhui inakaribia kumaliza kazi yake ya kupitia maudhui ya kipindi hicho.
chanzo: Mwananchi 

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment