Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani,
Pereira Ame Silima akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe
wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika
mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza
ajali za barabarani nchini. Kulia ni Katibu wa Baraza la Usalama Barabarani
ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu
Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga. Katikati ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la
Polisi nchini Malawi ambaye pia ni Kiongozi wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini humo, Maepheson Matowe. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na
Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Hoteli ya
Regal Naivera jijini Tanga leo. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mtoa mada wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa
Usalama Barabarani ambaye ni Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samweli Manyele
akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa
la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo
ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani
nchini. Prof. Manyele alitoa elimu ya jinsi ya kusafirisha salama kemikali.
Mkutano huo ambao unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama
Barabarani unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na
Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Pereira Ame Silima (katikati meza
kuu) akijadili jambo na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini,
Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga, wakati wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa
Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani
kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala
mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Wengine katika
picha ni wajumbe wa mkutano huo. Mkutano huo ambao unaenda sambamba na
Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Hoteli ya
Regal Naivera jijini Tanga leo. Picha
zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Wadau na Wajumbe wa Baraza la
Usalama Barabarani kutoka mikoa yote chini wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti
wa Baraza hilo, Pereira Ame Silima (hayupo pichani) katika mkutano wa baraza
hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za
barabarani nchini. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda
kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga
leo . Picha na Felix Mwagara, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
0 comments:
Post a Comment