Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika akiwasili katika Jengo la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako amewatembelea wagonjwa wa moyo leo. Kanu atakiwepo nchini kwa muda wa siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za kampuni na kijamii.
Aliyekuwa
mchezaji nguli wa timu ya taifa ya Nigeria au Super Eagles, Nwankwo
Kanu ambaye pia kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani
Afrika leo ametembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa lengo la kujua ni jinsi gani
taasisi hiyo inafanya kazi pamoja na kuwajulia hali wagonjwa wa moyo
waliolazwa katika Taasisi hiyo. pia
Akizungumza
baada ya kuwasili katika Taasisi hiyo Kanu ameelezea kuguswa na tatizo
la ugonjwa wa moyo hasa kwa watoto wadogo ambao amewatembelea na
kuahidi kubadilishana uzoefu kuhusu huduma za matibabu zinazotolewa na
wataalamu wa tasisi hiyo.
“Tatizo
la moyo ni kubwa sana kwa sasa na limekuwa likiongezeka kwa kasi lakini
cha kusikitisha ni kuwa sio kila mtu anaweza kumudu gharama za matibabu
yake. Hivyo basi kuna umuhimu mkubwa sana kwa serikali na wadau wengine
kuanzisha vituo maalumu kama hivi ili kuwasaidia wasiojiweza.” Alisema
Kanu
Katika
mazungumzo yake mchezaji huyo wa nyota wa zamani ambaye aliwahi kuwika
na vilabu kama vile vya Arsenal, Ajax na Inter Milan, amesema kuwa
pamoja na kuja kwa shughuli mbalimbali kama balozi wa kampuni ya
StarTimes lakini pia ana nia ya kushirikiana na watalaamu wa Taasisi
hiyo ya Moyo. Alielezea kuwa lengo ni kuwasaidia matibabu watoto wenye
matatizo ya Moyo ambao wazazi wao hawana uwezo na kwamba watazungumzia
suala hilo.
“Nimefarijika
sana kuona serikali ya watu wa Tanzania inachukua hatua stahiki katika
kuwasaidia wananchi wake. Pia ningependa kuchukua fursa hii kuwataka
watanzania hasa wanamichezo kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara
kwa mara kwani ukijua tatizo mapema ni rahisi kupata matibabu na kupona.
Tumeona mifano michache ya wachezaji maarufu mbalimbali barani Afrika
na kwingineko duniani wakifariki au kunusurika kufa wakiwa katika ya
mchezo kutokana na kutoweka wazi mustakabali wa afya zao.” Alihitimisha
balozi huyo wa StarTimes barani Afrika
Kwa
upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete, Dkt. Godwin Godfrey amelezea kuwa tangu Julai mwaka
jana mpaka sasa tasisi hiyo kwa kushirikiana na wataalam kutoka nje ya
nchi wamewafanyia upasuaji watoto zaidi ya 200.
Nwankwo
Kanu mbali na kujizolea umaarufu na heshima kubwa katika medani za soka
barani Afrika na Ulaya yeye pia alifanyiwa upasuaji wa moyo mwaka 1996
na ndipo alipoamua kufungua taasisi yake ya moyo inayoitwa “The Kanu
Heart Foundation.”
Taasisi
yake hiyo iliyoko nchini Nigeria ambako ndiko alipozaliwa aliianzisha
kwa madhumuni makubwa ya kusaidia wenye matatizo kama yake na ameahidi
taasisi hiyo kushirikiana na taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika
masuala mbalimbali.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo, Dk Peter Kisenge katika taasisi hiyo akimkaribisha Nwankwo Kanu Ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika. Kanu atakuwepo nchini kwa muda wa siku tano kushiriki shughuli mbalimbali za kampuni na kijamii.
Nwankwo Kanu ambaye pia ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika akimsikiliza Daktari bingwa katika Taasiai ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk Peter Kisenge wakati akitoa taarifa fupi ya taasisi hiyo
Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Nigeria, Nwanko Kanu akifafanua jambo kwa madaktari wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo hospitali ya taifa ya Muhimbili wakati alipotembelea hapo.
Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Nigeria, Nwanko Kanu akimsikiliza mmoja wa madaktari wakati alipotembelea katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo huku madaktari wa hospitali hiyo wakifuatilia mazungumzo hayo.
Mmoja wa wagonjwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ya hospitali ya taifa ya Muhimbili mtoto Mariam Omary akifurahi baada ya kupata fursa ya kutembelewa na kujuliwa hali na aliyekuwa mchezaji nyota wa nigeria, Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika.
Fatuma Shaban akipokea zawadi kutoka kwa aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Nigeria na kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika Nwankwo Kanu kwa niaba ya mtoto wake, Ramadhan Shaban ambaye amefanyiwa upasuaji wa moyo kwenye taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Aliyekuwa mchezaji nyota wa timu ya Taifa ya Nigeria Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni ya StarTimes barani Afrika akizungumza jambo na madaktari katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) alipotembelea taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ya hospitali ya taifa ya Muhimbili.
0 comments:
Post a Comment