Thursday 12 May 2016

#MICHEZO>>ENGLAND KUAMUA VITA YA HISPANIA UEFA.Fahamu zaidi hapa.

May 28 mwezi huu ndio fainali ya UEFA, mashindano yenye msisimko wa hali ya juu duniani kwa ngazi ya vilab ambayo itafanyika Italia katika mji wa Milan. Wakati hayo yakiendelea UEFA imemtangaza mwamuzi Mark Cluttenburg kuamua mechi hiyo kati ya majirani wasiopendana Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid.

KITUKO

 

Moja ya matukio yaliyompa umaarufu Clattenburg ni mechi ya kombe la ligi kati ya Liverpool na Reading ambapo alibaini hana kadi ya njano baada ya kutaka kumzawadia mchezaji wa Reading alipopapasa mfukoni hakuiona ndipo mwamuzi wa akiba akamletea nyingine na kutoa adhabu hiyo.

 

Mwaka huu inawezekana ikawa neema kwakwe kwani atachezesha fainali ya FA kati ya Manchester United dhidi ya Crystal Palace. Kisha atachezesha fainali ya UEFA Champions League. Hii inakumbusha Mwingireza  Howard Webb alichezesha fainali ya UEFA kisha fainali ya kombe la dunia.

 

Je naye atafika huko? kama unakumbuka mchezo kati ya Manchester United na Chelsea 2012 alipompa Torres kadi nyekundu kwa uzembe wake mwenyewe ambapo Torres alisukumwa lakini kadi akapewa yeye. Leo hii amekuwa mtamu kama mcharo kweli ukitulia utaweza kubadilika.


0 comments:

Post a Comment