Thursday 12 May 2016

#MICHEZO>>>YANGA NA AZAM USO KWA USO JUNI FAINALI YA FA.Fahamu zaidi hapa.

Fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga na Azam FC, imepangwa kupigwa Juni 11,2016 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Jamal Malinzi, amethibitisha hilo.

“Ratiba inaonyesha hivyo na hiyo tumefanya hivyo ili kuzipa muda wa kutosha wa maandalizi timu zote mbili kwasababu tuna fahamu zitakuwa zimetoka kumaliza mechi za ligi ya Vodacom nap engine nyingine zitakuwa na majeruhi na mapungufu mengine ya hapa na pale,”amesema Malinzi.

 

Chonde chonde Azam na Yanga hii ni fursa nzuri ya kuandika historia ambayo itaishi daima kwenye soka la bongo. Pia kocha Stewart Hall ni wakati wako sasa kuiaga Azam kwa kombe ili nawe ujitengenezee heshima kwenye klabu hiyo.


0 comments:

Post a Comment