Home »
Michezo
» #MICHEZO>>>KOCHA WA ESPARANCA ASEMA YANGA IMETUZOHOFISHA KUENDELEA KATIKA MCHEZO WA MALUDIANO.Fahamu zaidi hapa.
Kocha
mkuu wa Esparanca Zoram Manojlovec (kulia) amesema timu yake inanafasi
ndogo ya kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho ukilinganisha na
Yanga
Kocha wa GD Sagrada Esperanca Zoram Manojlovec anasema kipigo cha
magoli 2-0 walichokubali kutoka kwa Yanga kinawapa nafasi finyu ya
kusonga mbele kwenye michuano hiyo kwasababu kubadili matokeo wakiwa
Angalo itakuwa ni vigumu kwasababu Yanga watahitaji sare yeyote tu
ambayo itawafanya wafuzu kwenda kwenye hatua ya makundi ya kombe la
shirikisho.
“Kipindi cha pili Yanga walicheza vizuri sana na wakapata goli,
matokeo yangebaki 1-0 angalau tungeendelea kujipa moyo kwenye mechi ya
marudiano, lakini goli la pili limetumaliza. Tutacheza nyumbani mchezo
wa marudiano laiki matokeo ya kupoteza kwa goli 2-0 ni magumu kwetu.”
“Tuna dakika nyingine 90, inawezekana tukafanya jambo jambo ni vigumu
sana kwa upande wa timu yangu. Tulipotea kuanzia dakia ya 70, Yanga
wakapata nafasi ya kutufunga goli la pili kwa shuti la mbali, lakini
ndiyo mpira.”
“Ni ngumu kubalisha matokeo haya lakini inawezekana. Mfano mzuri ni
fainali ya Champions League kati ya Liverpool dhidi ya AC Milan walianza
kwa kupoteza kipindi cha kwanza kwa magoli matatu lakini Liverpool
wakasawazisha na kushinda kombe.”
Yanga ikiitoa Esparanca katika hatua hii, itakuwa imefuzu kwenda
hatua ya nane bora (hatua ya makundi) ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu
za Tanzania kufanya hivyo tangu Simba walipofuzu katika hatua hiyo
katika mashindano ya kbabu bingwa Africa mwaka 2003.
Related Posts:
MBAO FC INAAMINI ITAITWANGA AZAM FC NA KUBAKI LIGI KUU BARA.
Mbao FC ina uhakika wa kufanya vizuri na kubaki Ligi Kuu Bara na kazi hiyo inaanza kesho Jumamosi.
Mbao ina imani mechi yao dhidi ya Azam FC ugenini, tena usiku itakuwa ngumu lakini watafanfa vema.
“Itakuwa mechi ngumu… Read More
KIMENUKAA..Jengo la Yanga Kupigwa Mnada..Kisa Deni la Milioni.
JENGO la makao makuu ya Klabu ya Yanga lililoko makutano ya mtaa wa
Jangwani na Twiga Kariakoo jijini Dar es Salaam, liko hatarini kupigwa
mnada kutokana na deni la Sh. milioni 300 ambalo klabu hiyo inadaiwa,
imefahamik… Read More
Meneja wa AS Monaco anena na vyombo vya Habari hivi punde.Meneja wa AS Monaco Leonardo Jardi amesema kwamba, ni lazima washinde
katika mchezo wetu wa kwanza wa nusu fainali ya Klabu Bingwa Barani
Ulaya dhidi ya Juventus ili tupate nafasi ya kuingia hatua ya fainali.
Monaco itawa… Read More
EVERTON Yaja Kuzifunda Simba, Yanga Julai.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe,
amesema kikosi cha Everton FC kitatua nchini Julai mwaka huu kukipiga
dhidi ya Simba au Yanga katika mechi maalum zilizoandaliwa na serikali
ili kutanga… Read More
#PICHA>>>Mshambuliaji wa JKT Ruvu, Abdulrahman Mussa amekabidhiwa Tsh milioni 1 ikiwa ni zawadi Mchezaji Bora VPL kwa mwezi Aprili.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
&… Read More
0 comments:
Post a Comment