Midfielder wa Manchester United Bastian Schweinsteiger anajiandaa kucheza tangazo jipya la iPhone app, Clash of Kings.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani akiwa na kikosi cha Old Trafford ndani ya msimu wake wa kwanza kwenye Premier League hajafurahia maisha yake mapya kwenye ligi hiyo kutokana na kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara huku kukiwa na taarifa huenda akaikosa michuano ya Euro itakayoanza mwezi June nchini Ufaransa.
Kiungo huyo mwenye miaka 31, anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi katika maisha yake ya soka na muda huo atautumia ku-shoot tangazo jipya la Clash of Kings.
Kwa mujibu wa gazeti la Bild la nchini Ujerumani, Schweinsteiger atacheza kama King kwenye tangazo hilo la kibiashara huku akiwataka watu wa- in stall app hiyo ya game na kucheza.
Bado haijawekwa wazi kwamba ni lini tangazo hilo litaachiwa lakini itakuwa inavutia kumuona Schweinsteiger kwenye sehemu ya tangazo hilo.
Je atafuata nyayo za mchezaji wa zamani wa Manchester United Eric Cantona kuamua kucheza movie baada ya kutundika daruga? Tusubiri tuone nini kitatokea.
0 comments:
Post a Comment