Nyota wa muziki wa Rap Bongo ‘Rhymes Of Magic Attraction’ Roma 
amethibitisha fununu za kuwa muziki anaoufanya umekua ni msalaba mzito 
kwenye maisha yake.
Akizungumza na eNewz Roma alisema kuwa hayo ndiyo maisha 
aliyoyachagua na ni mwanaharakati anaetetea haki na amani katika taifa 
lake, maendeleo bora na hicho ndicho kitu kikubwa anachojaribu 
kukipigania.
“Natamani nipate utawala au uongozi ambao utamfanya Roma asiimbe hip hop na ukiona kila siku Roma anatoa mawe basi ujue bado hatujapata uongozi huo ama utawala huo,” alisema Roma na kuongeza, “Kwa hiyo inabidi niendelee kushindilia ili taifa langu siku moja lione kwamba Roma alikuwa ni mmoja kati ya wapigania haki”.

0 comments:
Post a Comment