RAIS
 John Magufuli ametakiwa kutumbua majipu ya wanasheria walioshindwa 
kumshauri kufuata sheria ya kukasimisha mamlaka ya kiuwaziri kwa 
mawaziri walioteuliwa miezi sita iliyopita.
Tundu
 Lissu amesema hayo Dodoma wakati akitoa maoni kuhusu Mpango na 
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya wizara ya Sheria na Katiba 
kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017, Bungeni mjini Dodoma.
“Kwa
 kuangalia mifano ya matangazo mbalimbali ambayo yametolewa na 
watangulizi wa Rais Magufuli tangu sheria ya utekelezwaji wa majukumu ya
 kiuwaziri ilipotungwa mwaka 1980, hata mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa
 kwanza angeweza kumtengenezea draft ya Tangazo la aina hiyo,” amesema Lissu.
Ameongeza “iweje
 watu wenye Shahada za uzamivu na uzamili katika sheria washindwe 
kufanya hivyo kwa karibu ya nusu mwaka tangu wateuliwe? Kama ni majipu 
ya kutumbuliwa na Magufuli, basi wasomi hawa wa sheria ni majipu na 
wanastahili kutumbuliwa.”
“Kwa
 sababu Rais Magufuli sio mwanasheria, amemteua Mwansheria Mkuu wa 
Serikali ambaye kwa mujibu wa ibara ya 59(3) ya katiba ndiye mshauri wa 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya kisheria,” amesema Lissu.
Kwa
 sababu hiyo, Rais Magufuli amemteua Dk. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri 
wa Katiba na Sheria ili awe mshauri wake mkuu katika utekelezaji wa 
madaraka yake katika masuala ya kikatiba na kisheria kwa mujibu wa ibara
 54(3).
“Kwa
 bahati nzuri Rais amewateua Dk Harrison Mwayembe, Dk Sifuni Mchome, na 
Amon Mpanju kuwa viongozi wa Wizara ya Katiba na Sheria ambao wote 
wasomi wabobezi wa sheria,” amesema.
Amehoji kuwa “Kambi
 ya Upinzani ianataka kupata majibu sahihi ni kwa nini wanasheria 
wabobezi wote hawa wameshindwa kumshauri Rais Magufuli kutoa tangazo la 
kukasimisha majukumu ya kiuwaziri kwa mawaziri mbalimbali aliowateua 
miezi sita iliyopita?”
Amesema
 kila mtu anafahamu kwamba Rais sio mwanasheria lakini kutokuwa 
mwanasheria haimaanishi kuwa juu ya sheria bali anapaswa kufuata sheria 
za nchi.
Lissu
 amesema, maana na athari ya kisheria ya kutokuwepo kwa tangazo la 
ukasimishaji wa majukumu ya kiuwaziri ni kubwa kutokana na kwamba 
mawaziri walioteuliwa wamefanya mambo makubwa mengi ambayo yalikuwa 
kinyume cha sheria.
 









 




 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment