JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa
kutakuwa na Semina ya wiki moja ya Wakuu wa Kamandi wa majeshi ya Nchi
kavu Afrika itakayoendeshwa Mkoani Arusha katika Hoteli ya Mount Meru
kuanzia tarehe 13 hadi 19, Mei 2016.
Lengo
la Semina hiyo ni kuwakutanisha Wakuu wa kamandi hizo Afrika ili
kujadili na kuendeleza ushirikiano katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo
mbalimbali yanayolikabili bara la Afrika katika Nyanja ya ulinzi.
Kauli Mbiu ya Semina hiyo ni Ujenzi wa Usalama Afrika kupitia Ushirikiano.
Semina
hii hufanyika kila mwaka katika mojawapo ya nchi za Afrika, ili
kuwajengea makamanda hao ushirikiano katika kutatua changamoto
mbalimbali za kiulinzi zinazotokana na mabadiliko katika Nyanja za
kiusalama.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
0 comments:
Post a Comment