Watumiaji
wa smartphone au maarufu Simu-Janja ni watu makini sana linapokuja
suala la ukubwa wa simu, mwenendo wa masoko kwa sasa unaonyesha
wanunuaji wengi wa simu wanavutiwa sana simu zenye kioo kipana.
Lakini
sio wapenzi wote wa simu wanatamani simu zenye kioo kipana, watumiaji
wengine wanapenda simu zenye ukubwa wa wastani. Fununu zilizotapakaa ni
kuwa TECNO wanakuletea simu mpya Phantom 6 ambayo pia itakuja na matoleo
mengine kama Phantom 6 Plus na Phantom 6 mini.
Fununu
hizi zinaweka wazi kwamba watengenezaji hawa wakubwa wa simu za mkononi
wana mkakati kabambe wa kuwavutia watumiaji wakubwa wa simu kununua
matoleo haya mapya yanayotarajiwa kutoka Septemba hii pindi TECNO
Phantom 6 itakapazinduliwa.
HAKUNA SHAKA JUU YA UKUBWA WAKE
Jambo
hili linatia moyo huku TECNO ikiwekwa bayana katika uvumi unaosambaa
angalau kwa vidokezo na muonekano ambao unasemekana ni rasmi Tecno
Phantom 6 itaboreshwa zaidi na wala haitopunguziwa sifa zake kuu.
Nafikiri
hili ni jambo la kufurahisha sana kwa sababu mara nyingi tumekuwa
tukiona makampuni mengi ya simu yakiwauzia wateja wao simu zenye uwezo
mdogo katika maduka yao makubwa wakitumia jina la makampuni yanayobamba
kwa kuuza simu. Watumiaji wengi wa simu siku hizi wako makini sana na
hawadanganyiki kirahisi.
PHANTOM 6 NA MATOLEO MAPYA YA TECNO YATAKUWA NI GUMZO?
Watengenezaji
hawa wakubwa wa simu za TECNO wamekuwa wakipambana kuweka toleo lao
bora kabisa kwenye mauzo kuanzia Phantom A+ mpaka Phantom Z au Z mini,
Phantom 5 na sasa Phantom 6. Swali linalobaki ni je, phantom 6
itabadilisha mtazamo wa baadhi ya wananuaji wa simu?
Unadhani
wpenzi wa Smartphones wataanza kuiona Phantom 6 kama moja ya toleo la
kipekee kama inavyotarajiwa na wengi? Na inasemekana kuwa Phantom 6 ama 6
+ itakamata soko kubwa kipindi hiki endapo toleo zitambulishwa kwa
upekee kwa wakati muafaka.
Mbali
na fununu zote hizi tunasubirri kuona toleo rasmi la Phantom 6
kuzinduliwa ifikapo Septemba. Endapo unahitaji taarifa zaidi unaweza
kutembelea mitandao ya kijamii ya Tecno kama ilivyoorodheshwa hapa
chini.
Twitter: https://twitter.com/TECNOMobileTZ
0 comments:
Post a Comment