Sina tatizo na hatua za Raisi kuleta 'maendeleo' kwa wananchi na kutetea 'wanyonge'. ILA nina tatizo na kauli zake. Kuna jinsi ambavyo kama watanzania tumezoea kusemeshana na kuongeleshana. Sisemi kwamba tuishi kwa mazoea la hasha. Ila ni vyema mtu yeyote uangalie unasema nini na wapi kufanikiwa nini.
Mlimani City mpango wa kuijenga ulianza kipindi cha Mh. Mkapa na kumalizika kipindi cha Mh. Kikwete kama sikosei. Leo hii kusema kwamba mradi huo ni "magodown" ni kuwaonea waliokuwepo wakati unatekelezwa.
Mosi, maamuzi ya Serikali yeyote ni ya pamoja (collective responsibility). Kama mtu alikuwepo kwenye mabaraza yote ya mawaziri kipindi cha Mh. Mkapa na Mh. Kikwete kipindi ambacho magodown yamejengwa basi hawezi kuepuka ushiriki katika kudanganywa kwetu!! Pili, sijamsikia mtu akisema barabara ambazo zimebomoka (mfano maeneo ya Chalinze, barabara ya Mbeya, barabara za akachube nk) ni mitaro au mito kwa sababu zilijengwa chini ya kiwango!! Au ule mradi wa ferry kutoka Bagamoyo - Dar ni WHITE ELEPHANT. Au kukumbushia uuzaji wa nyumba za Serikali halafu kwenda kujenga nyingine!! Au kuhusu wale samaki wa wachina kwamba tuliingizwa chaka.
Tatu, uongozi ni endelevu. Zaidi pale ambapo bado ni CCM ndio kipo madarakani. Inatuchanganya wananchi tunapoambiwa tulichezewa na kudanganywa sana huko nyuma. Nyuma tunayoijua sisi ni ya NYERERE, MWINYI, MKAPA na KIKWETE. "Nyuma" ya CCM. Je ni yupi kati yao alikuwa mzembe na asiyejua kuongoza kiasi kwamba leo hii tuko hapa na magodown yetu???? Atuombe msamaha!! Kwa njia moja au nyingine ni ukweli kwamba sisi watanzania ni majuha. Tumechezewa wakati wa hao wote wala hatukujua. Leo angalau ametokea mtu kutuambia ukweli. Mzee Mkapa alikuwa sahihi kutuita malofa.
Lakini najaribu kujiamiaminisha kwamba Mh. Raisi ni mtu wa kauli za utani. Mfano, 1. Kufyatua watoto 2. Siasa mpaka 2020 3. Kuwapoteza nusu walioimba kwenye mkutano 4. Kumzamisha kisimani aliyezuia watu kuchota maji 5. Kutoa matairi kwenye magari yanayovunja sheria za barabarani 6. Polisi kutokuwa rafiki na raia 7. Kutokusaini pensheni mtu asipokupa mkono wa salamu nk nk.
Natamani sana niamini hivyo. Ni utani tu. Naomba sana iwe hivyo. #TatizoNiSisi
Alberto Msando
0 comments:
Post a Comment