TWITE (KULIA) AKIWA NA JUMA ABDUL
Beki nyota wa Yanga, Juma Abdul, amesema ni vigumu kusahau mchango wa kiraka Mbuyu Twite ambaye ametupiwa virago ili kumpisha Mzambia, Justine Zulu, kwani alikuwa ni zaidi ya mchezaji kikosini mwao.
Rasmi
Twite ameondolewa kwenye kikosi huku Zulu maarufu kama Mkata Umeme
akianza kuitumikia timu, lakini Juma Abdul anaamini Twite alikuwa injini
ya mafanikio kwa kipindi alichokaa Jangwani kutokana na umahiri wa
kucheza zaidi ya namba moja, jambo ambalo liliisaidia Yanga kwa sehemu
kubwa.
Ikumbukwe
Mnyarwanda huyo mwenye asili ya DR Congo, alihimili kucheza namba zote
kwenye safu ya ulinzi, kiungo mkabaji ama kuchezesha timu, hivyo kuwa
hazina kubwa ya Yanga.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam beki huyo wa zamani wa Mtibwa, alisema: “Twite
kiukweli tutamkumbuka kwa mengi, pamoja na maelewano uwanjani, lakini
uwezo wake wa kucheza karibu kila namba uliisaidia sana timu.
"Hakika
huwezi kuzungumzia mazuri ya Yanga kwa kipindi alichokuwepo bila
kumtaja alikuwa akiiokoa timu mara kadhaa wakati anapokosekana mchezaji
yeyote hata mimi.”
Source: Championi
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment