QADAFFI ANAANZA HIVI: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema....
Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa
nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na
shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi
kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.
Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani),
alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini
akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu
waafrika fedha kupitia AU.
Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya
demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.
Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.
Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia
Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa
"demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye
nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.
Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa
hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure
na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).
Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.
Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo
waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na
kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.
Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua
naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili
kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.
Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika
historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.
Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya,
huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa
kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"
Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa
"washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia
kuteseka.
Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.
Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula
bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha
tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.
Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!
Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi
wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na
nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka
na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.
Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi
kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu
ya utoto kule Sirte.
Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua
Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa
ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.
Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua
ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee
kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya
kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu
wangu.
Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru.
-- Mu'uammar Qaddafi.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment