Mapenzi ni nini? Kuuliza swali hili kwa mtu yeyote atakupa majibu
yasiyokuwa na kikomo. Mapenzi ni dhana pana ambayo kila mtu anakuwa na
mtizamo tofauti wa kueleza.
Kiufupi mapenzi ni jambo lisiloeleweka, jambo lisilo na mwisho. Na kwa
kuwa mpenzi wako anachangia pakubwa katika kuyaendeleza mahusiano yenu
yawe marefu ya kufaana, furaha, na hata kukuwezesha kuwa na maisha bora,
tumekuja na tafiti tulizilokusanya kukupa sababu za kisaikolojia ambazo
zinachangia wapenzi wawili wapendane.
Ok, kabla ya kuorodhesha orodha nzima je ulikuwa ukijua kuwa homoni
zako, maslahi, na hata sura ya mzazi wako inachangia pakubwa kwa
kumchagua yule ambaye atakuwa mpenzi wako?
Zama nami...
Sababu za kwa nini watu huangukia katika mapenzi
1. Kama mnafanana ile sana
Tafiti zinaonyesha ya kuwa ile dhana ya kuwa "watu tofauti huvutiana"
haina msingi. Badala yake wale watu ambao wanagawa mambo mapana, kama
vile hulka, wana urahisi wa kuhisi sawa katika maisha yao ya kila siku.
Utafiti huu uliweza kuthibitishwa na Gian Gonzaga, mwandishi mkuu katika
eHarmony. Utafiti huu ni wa uhakika kwani katika maisha ya kawaida ya
mapenzi, iwapo wapenzi wanagawa hulka, moja maisha yao ya kimapenzi huwa
marefu na ya kufaana.
2. Kama unafanana kama mzazi wake
Kulingana na mwana saikolojia David Perrett kutoka chuo kikuu cha St.
Andrews amegundua ya kuwa watu huvutiwa na jinsia ile nyingine ambayo
wana nywele na rangi ya macho ambayo ni sawia na ya mzazi wake wa ile
jinsia tofauti. Pia katika tafiti yake amegundua kuwa "wanawake ambao
walizaliwa na wazazi ambao ni 30+ hawavutiwi sana na wanaume vijana ila
wale wakubwa, tofauti na wanawake waliozaliwa na wazazi wadogo." Katika
wanaume, Perrett alikiri kuwa kuchagua mpenzi kisura kwa mwanaume
kunachangiwa pakubwa na umri wa mzazi wake wa kile.
3. Kama unanukia ipasavyo
Katika mapenzi, chuo kikuu cha California kilifanya utafiti kikagundua
ya kuwa mwanamke ambaye ameingia siku zake ya uzazi (ovulating) huwa
wanapenda na kuvutiwa sana na harufu ya tsheti iliyovaliwa na mwanaume
ambaye ana kiwango kikuu cha homoni za testosterone. Pia wanawake hao
hao walikiri kupenda wanaume ambao wana taya ndefu.
4. Kama utawacha mikono yako na kifua chako wazi
Kuweka mikono yako ndani ya mifuko na kuyaweka mabega yako ndani unatoa
ishara ya kuwa hujiskii kuongea. Lakini iwapo unaongea huku mikono yako
umeiweka wazi na kusimama wima kifua mbele kunaonyesha ya kuwa ukotayari
kwa lolote lile.
5. Kama mtaangaliana machoni kwa dakika mbili
Wakati mwanasaikolojia Joan Kellerman katika chuo kikuu cha
Massachusetts alipowaagiza wanafunzi 72 wawili wawili waangaliane kwa
dakika mbili mfululizo, waliripoti kuongezeka kwa hisia za upendo na
mapenzi kwa huyo mwenzake. Hii ni idhibati tosha ya kuonyesha ya kuwa
muda mrefu wa kuangaliana macho kunaweza kukakuunganisha na mtu na hata
kuchangia hisia za mapenzi.
6. Kama unamiliki mbwa
Katika majaribio katika chuo kikuu cha Michigan, wanawake hupenda kusoma
tabia za wanaume. Iwapo kuna habari ambayo inahusisha mwanaume ambaye
anamiliki mbwa, wanawake wanampa kiwango cha juu cha uhusiano mrefu wa
kuvutia. Hii ni kwa sababu watafiti walivumbua ya kuwa umiliki mifugo wa
nyumbani inaweza kuwa ishara ya mtu ambaye ni mmakinifu na mwenye kuwa
na hulka ya kupenda kujitweka majukumu katika mahusiano.
7. Kama unacheza mziki
Watafiti katika nchi ya Ufaransa wamegundua kuwa uhusisho wa mziki
kunahusiana na uchaguzi wa mapenzi. Katika majaribio, mwanaume aliyebeba
gita ama begi la mchezo aliuliza wanawake 300 namba zao za simu.
Mwanaume aliyebeba gita aliweza kupewa namba nyingi zaidi kuliko
alipobeba begi la mchezo.
8. Kama utavalia nguo nyekundu
Katika utafiti uliofanywa Slovakia, wanawake ambao walivalia nguo za
rangi nyekundu walifanikiwa zaidi katika mchezo wa kufanya mapenzi. Hii
ilichangiwa pakubwa na ishara ya kuwa nguo nyekundu wanawake wengi
wanaitumia kama njia ya kuwavutia wanaume wenye uwezo.
9. Kama una nywele flani katika uso wako
Katika utafiti wa mapenzi uliofanywa nchini Australia uligundua kuwa
wanawake huvutiwa zaidi na wanaume ambao wana ndevu wastani katika uso
wao. Waligundua kuwa mwanaume mwenye ndevu nyingi ama ambaye amenyoa uso
mzima hawavutii kwao. Pia watafiti waligundua kuwa mwanaume mwenye
nywele nyingi zaidi, huonekana na wanawake kuwa kiume zaidi.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment