Saturday 14 May 2016

#MICHEZO>>>>PELLEGRINI AMUONYA GUARDIOLA.Fahamu zaidi hapa.

Meneja wa  Manchester City anayemaliza muda wake Manuel Pellegrini, amemuonya vikali Pep Guardiola ambaye ndiye atakayechukua mikoba yake kunako klabu hiyo juu ya kuwa na matarajio makubwa katika msimu wake wa kwanza kunako Ligi kuu ya England msimu ujao.

Guardiola anatarajia kuondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu, na kujiunga na Manchester City kwa mantiki ya kuifanya Manchester City kuwa moja ya miamba ya soka barani Ulaya.

Pellegrini anaondoka wakati akiwa amechukua mataji kadhaa nchini England kama Ligi Kuu nchini humo, Kombe la FA, kombe la ligi pamoja na kufanikiwa kuifikisha City kwa mara ya kwanza hatua ya nusu fainali UEFA msimu huu, ambapo walitolewa na Real Madrid.

Amesema hakuna kitu rahisi kwenye ligi kuu England, huku akijiandaa na mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu dhidi ya Swansea na kuonya kuwa kwa mara ya kwanza Guardiola atakuwa kwenye mtihani mkubwa sana katika maisha yake ya kufundisha soka.

“Bilashaka ni changamoto kubwa pale unapokuja kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu England”, alisema Pellegrini.

“Hapa simzungumzii Guardiola, najizungumzia mwenyewe, wakati nilipofika kwa mara ya kwanza kabisa”.
Amesema kwamba mahitaji ya Ligi Kuu England ni makubwa zaidi kutokana na uhalisia kwamba kila mchezo katika ligi hiyo una ushindani mkubwa ukifananisha na ligi nyingine.

0 comments:

Post a Comment