Friday, 6 May 2016

#MICHEZO>>>WAAMUZI KUTOKA GHANA KUAMUA MECHI YA YANGA CAF.Fahamu zaidi hapa.

MWANDISHI WETU

Mwamuzi Joseph Odartei Lamptey, Jumamosi Mei 7, 2016 anatarajiwa kuwa mwamzi wa kati katika mchezo wa kimataifa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaozikutanisha timu za Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na GD Sagrada Esperanca ya Angola.


Lamptey kutoka jiji la Accra, Ghana atasaidiwa na raia wenzake wa nchi hiyo kuchezesha mchezo huo Na. 99. Mwamuzi Msaidizi Na. 1 (line 1) ni David Laryea wakati Mwamuzi Msaidizi Na. 2 (line 2) ni Malik Alidu Salifu.


Mwamuzi Msaidizi mezani (Fourth Official) ni Cecil Amately Fleischer huku Kamishina wa mchezo huo, akiwa ni Asfaw Luleseged Begashaw wa Ethiopia.


Viingilio na upatikanaji wa tiketi unatarajiwa kutangazwa leo baada ya mkutano kati ya makocha wa timu zote mbili. Mkutano wa makocha hao utafanyika saa 5.00 mchana kwenye Ukumbi wa mikutano wa TFF.


0 comments:

Post a Comment