Aliyekuwa
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya, Sioi
Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic tawi la
Tanzania ambaye pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose
Sinare wamefika Mahakama kuu leo May 06 2016 ili kusikiliza rufaa ya
kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.
Rufani
hiyo imesikilizwa leo ambapo mahakama kuu imefuta pingamizi hilo
kutokana na kuwa na dosari hivyo shauri linarudi kwenye mahakama ya
hakimu mkazi Kisutu kuendelea pale lilipokuwa limeishia na upande wa
Jamhuri wanaweza kuandaa tena rufani na kufungua tena.
Serikali
ilikuwa imekata Rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu
kuwafutia washitakiwa shitaka la kutakatisha pesa ambalo liliwafanya
wanyimwe dhamana.
Baada ya shitaka hilo kufutwa, watuhumiwa sasa wanaweza kuomba dhamana.
0 comments:
Post a Comment