Aliyekuwa kiongozi Mkuu wa Upinzani katika uchaguzi mkuu nchini Uganda huenda akahukumiwa kifo kama akikutwa na hatia ya mashtaka yanayomkabili.

Kizza Besigye Kifefe anashtakiwa kwa kosa la uhaini nchini Uganda baada ya kujiapisha na kujitangaza kuwa yeye ndiyo Rais wa Uganda siku moja kabla Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni hajaapishwa kushika wadhifa huo.

Hukumu ya kosa la uhaini (kupindua serikali) ni kifo. Hivyo suala hili limezua sintofahamu kama kiongozi huyo wa upinzani atahukumiwa kifo kama akikutwa na hatia.

Wataalamu wa sheria nchini Uganda wanasema kua nafasi ya Kizza Besigye kushinda kesi hiyo ni ndogo sana kutokana na kile walichosema kuwa alitangaza hadharani nia yake ya kutaka kuipindua serikali ya Uganda.

Kizza Besigye ambaye amekuwa akikamatwa mara kwa mara tangu harakati za uchaguzi kuanza nchini Uganda ameshtakiwa katika mahakama ya Moroto, Uganda.

Kizza Besigye alijiapisha siku ya Jumatano Mei 11 na kusema ana kila nyaraka inayothibitisha kuwa yeye alishinda uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Februari