Saturday, 13 May 2017

KAZI YA SERENGETI BOYS GABON INAANZA JUMATATU, ANACHOAMINI SHIME HIKI HAPA.

Kocha wa timu ya taifa vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Bakari Shime amesema watahakikisha wanapata ushindi dhidi ya Mali  katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) utakaochezwa keshokutwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Port Gentil, Gabon.


Serengeti imepangwa Kundi B sambamba na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Mali, Niger na Angola na inahitaji kushinda michezo miwili ili iweze kufuzu katika fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika mwaka huu nchini India.


Akizungumza kutoka Gabon, Shime alisema kikosi chake kipo tayari kuingia vitani katika michuano hiyo kutokana na maandalizi makubwa waliyofanya hivyo ana imani kubwa watashinda mchezo huo.


 “Tunashukuru kila kitu kinaenda vizuri hakuna mchezaji yeyote majeruhi tunachosubiria ni kuanza kwa michuano, naamini mechi saba tulizocheza za kirafiki zimetoa mwanga mkubwa kwa uelekeo wa timu yetu katika michuano hii.

 “Hatuwezi kuwahofia Mali kwa sababu moja kati ya timu ambazo zinatajwa kuwa ni ngumu Serengeti Boys ipo, kikubwa ambacho tumekifanya ni kuwaondoa woga vijana wetu.

“Tumewaongezea hali ya kujiamini kwa sababu hii ndiyo michuano tuliyokuwa tunaipigania kupata nafasi, naamini kwamba Mali tutawafunga kikubwa Watanzania waendelee kutuombea,” alisema  Shime.

MECHI ZA SERENGETI
Jumatatu Mali v Serengeti
Mei 18, Serengeti v Angola

Mei 21, Serengeti v Niger
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment