Jeshi la Polisi limefanikiwa kumtia nguvuni  Tabibu Juma Mwaka, maarufu Kama Dokta Mwaka (Pichani), baada ya kumsaka Kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Jeshi la polisi lilikuwa likitekeleza agizo la Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuwa tabibu huyo mashuhuri akamatwe Kwa kukiuka agizo la Serikali la kuacha kutoa huduma za tiba asili na tiba mbadala baada ya kufutiwa kibali na Baraza la tiba asili na tiba mbadala.

, ambao walimkuta na hatia ya kukiuka masharti ya sheria ya tiba asili na tiba mbadala ya Mwaka 2002, sheria namba 23, ulaghai wa kujiita dokta na kujifanya amesomea tiba ya kisasa kumbe la, kukutwa na shehena ya dawa za kisasa zaidi ya boksi 200 bila vibali vya mamlaka ya chakula na dawa, TFDA na kukutwa na shehena ya dawa za tiba asili na tiba mbadala kinyume cha sheria, haswa baada ya kufutiwa usajili wa kutoa huduma hizo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia jioni hii zinaeleza kuwa, Tabibu Mwaka anashikiliwa na polisi Kwa mahojiano katika kituo cha Polisi Kati Jijini Dar es Salaam.. Kwa taarifa zaidi tutaendelea kuwajulisha kadri ya uwezo wetu.