Siku za hivi karibuni, habari ya town katika michezo ni uamuzi
wa wanachama wa Yanga kuamua kuikodisha timu yao pamoja na nembo kwa
Mwenyekiti wao Yusuf Manji ambaye pia ni Mwenyekiti wa klabu hiyo kongwe
zaidi nchini.Kutokanana hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul
Makonda yeye aliandika maneno ambayo yalizua utata kwenye mitandao ya
kijamii: Unataka kujua kwanini Tanzania ni masikini? Soma mkataba wa
Yanga wanaosaini leo.”Makonda ametolea ufafanuzi post yake wakati
akizungumza na kwenye kipindi cha Sports Extra cha Clouds FM ambapo
ameeleza kwa nini
aliandika ujumbe huo. Ungana na Makonda hapa chini
upate kuelewa vizuri alichokimaanisha katika ujumbe huo ambao ulizua
mjadala na maswali mengi mitandaoni, lakini inawezekana wengi walielewa
tofauti na alivyomaanisha.
Nilivyosikia namna ambavyo watu wanawaza kukodishana, nililazimika kutafuta uelewa kidogo. Kwasababu nilipata shida kidogo, mimi mwenyewe mbali na kuwa mkuu wa Mkoa, kama mwananchi wa kawaida anayependa michezo nimejikuta ninamaswali mengi .
Niliangalia kipindi cha Clouds TV (Sports Bar) wakati wanafanya mahojiano na Makamu Mwenyekiti wa Yanga, nikawa na shauku ya kumuuliza lakini nilivyomsikiliza mwanzo hadi mwisho namna alivyokuwa akijibu maswali nikagundua nikimuuliza maswali ndugu yangu nitakuwa namuonea.
Nikajiuliza nitapeleka wapi maswali yangu? Lakini nikawa najiuliza wanachama wamepata nafasi ya kupitia vizuri hiyo proposal? Kamati ya utendaji imepata nafasi ya kuipitia? Kwa bahati nzuri mzee wangu mzee Jakaya Kikwete ni mwanachama mzuri wa Yanga, nikajiuliza mzee nae amepata nafasi ya kupitia? Nikaendelea kujiuliza hawa watu wamepata kujua kama timu yao inakodishwa?
Bado nikajiuliza, anayeongoza ndio huyohuyo anaetaka kukodi klabu, je amezingatia uzalendo wa ahadi ambazo aliwahi kuzitoa juu ya klabu yake?
Watu wanaweza kuona tunaijadili Yanga kwasababu labda kwasababu wengine tunaonekana ni Simba, shauku yangu mimi kama Makonda, hizi timu zetu mbili zina sura nzuri sana na ndio zenye mwamko wa michezo Tanzania ukiongelea Simba na Yanga ni timu kubwa zina fan base kubwa. Hivi juzi tumeona Simba wameadhimisha miaka 80 maana yake wapo kwa miaka nenda rudi.
Lakini kama ndugu zetu weli wanania njema, kwanini wasifanye kama Bakhresa wakaanzisha timu zao kwanini waje wachue timu zilizotengenezwa miaka nenda rudi na zenye historia kubwa wanakuja kuzichukua hapa juu.
Kwahiyo kuna maswali mengi, ambayo mimi ningeoma wanayanaga na hata wanasimba pia wachukue nafasi nzuri na nimwombe MO ambaye anataka kuchukua shea Simba na Manji ambaye anataka kuikodi Yanga kwa miaka 10 wawape muda wanachama.
Wakati mnagombea nafasi za uongozi katika hizi timu kuna mambo ambayo mliyaahidi kwamba mtayatekeleza, lakini mbona bado tunatafuta kiwanja cha Yanga kimejengwa wapi, makao makuu ya Yanga lini yameboreshwa, lini jezi za Yanga zimeuzwa na zikaongeza mapato, wanachama wa Simba na Yanga lini wamelipa michango yao ya uanachama, hayo yote hatuyaoni.
Kwa bahati nzuri kaka yangu Nape naamini atatusaidia, tuna TFF ambayo ipo kwa ajili ya kusimamia hizi taratibu, hebu tupate kitu kizuri, tusikimbilie kufanya maamuzi ambayo kesho na keshokutwa tukaja kujutia, ninahisi kwa mbali sana kuna harufu ya ‘RICHMOND’.
0 comments:
Post a Comment