Mke
wa Rais, Janeth Magufuli amewaomba viongozi kusimamia na kuhakikisha
misaada yote inayotolewa kwa ajili ya wazee na watu wenye mahitaji
maalumu inawafikia walengwa.
Pia,
alimsifu mhubiri wa Nigeria, TB Joshua kwa kujitoa katika kuwasaidia
wazee na watu wasiojiweza nchini huku akiitaka jamii iige mfano huo.
Mama
Magufuli alisema hayo alipokuwa akitoa misaada katika Kituo cha Kaseka
cha Wazee na Walemavu wa Ukoma kilichopo wilayani hapa Mkoa wa Mtwara.
“Niombe
viongozi waliopo hapa kuhakikisha walengwa wanafaidika na misaada
wanayopata, tayari nimepata malalamiko mengi kutoka kwa Wasukuma
wenzangu kule Mwanza, yanavunja moyo.
‘‘Naomba
watu wasiuze wala kuiba ni dhambi kubwa ukichukua chakula cha mtu
mwenye mahitaji na asiyejiweza hiyo laana itakufuatilia kwa sababu ni
sadaka ishaombewa,” alisema.
Mama
Magufuli kwa kushirikiana na Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa
walikabidhi misaada mbalimbali ikiwamo vyakula, nguo, saruji, vitanda na
magodoro ambavyo vimetolewa na TB Joshua, kampuni ya Super Doll,
Dangote na viongozi wanawake wa Mkoa wa Mtwara.
“Niombe
wizara, taasisi, Serikali na mashirika ya ndani na nje kuiga mfano wa
TB Joshua kwani hakuangalia utaifa wala dini, uwapo wetu hapa unaonyesha
ni namna gani nchi na mila zetu za Kitanzania zinavyothamini na
kuheshimu wazee na watu wenye mahitaji maaalumu,” alisema Mama Magufuli.
Mwenyekiti
wa wazee hao, Cosmas Mbego aliwashukuru waliotoa misaada hiyo akisema
wanashangazwa kwani hawakuwahi kutembelewa na wake wa viongozi
waliopita.
“Lakini niseme ukweli maji huwa hatupati. Mlipokuja ninyi yanatoka lakini mtakapoondoka watayafunga,” alisema Mbego
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego aliwahakikishia wazee hao kuwa tatizo
la maji limeondoka na watakapoondoka yataendelea kutoka.
0 comments:
Post a Comment