Mwenyekiti
wa Yanga, Yusuf Manji ameeleza namna alivyosimamisha uanachama wa
baadhi ya wanachama wa Yanga wakiwemo wachezaji wa zamani kama Bakari
Malima ‘Jembe Ulaya’ na Aaron Nyanda.
Nyanda
na Malima ni wachezaji wa zamani wa Yanga ambao walikuwa kati ya
waliochukua fomu za kuwania uongozi kupitia uchaguzi wa Yanga
ulioandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliopangwa Juni 25.
MALIMA
Mwingine
aliyevuliwa uanachama ni anayejulikana kuwa ni Mwenyekiti wa Matawi wa
Yanga, Mohammed Msumi, cheo ambacho uongozi chini ya Manji umekuwa
ukisisitiza hakipo kikatiba.
Lakini
Manji akaeleza kulikuwa na njama za kumng’oa na kumuondoa zilizokuwa
zikifanywa na baadhi ya wanachama wakiwemo baadhi ya maofisa wa TFF.
“Kweli
nimewavua uanachama baada ya kugundua njama hizo. Kamati husika ya
Yanga ambayo ni ile ya nidhamu itakaa na kulifanyia kazi hili.
“Kama itaona kuna tatizo, itakazia nilichokitangaza. Kama hawana tatizo, basi itabadili, tuiachie kamati,” alisema Manji.
NYANDA
Manji
pia aliungana na wanachama waliungana kuwasikiliza sauti za watu
aliowatuhumu kuwa ni baadhi ya wanachama wa Yanga na maofisa wa TFF
waliokuwa wakipanga njama za kumng’oa kwa makusudi.
0 comments:
Post a Comment