Baadhi
ya wanawake wanaojiuza katika mitaa ya Majengo B na Fisi, mjini Mpanda
mkoani Katavi wameitaka Serikali kuandaa utaratibu wa kuwatambua ili nao
waweze kulipa kodi na kuliingizia taifa pato kutokana na shughuli
wanayofanya ya kuuza miili yao.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti jana usiku, baadhi yawanawake hao walisema
wanafanya kazi kama zilivyo kazi nyingine kwani zinawaingizia kipato
kizuri kinachowasaidia kutimiza mahitaji yao ya msingi hivyo kazi hiyo
inapaswa kuheshimiwa na kutambuliwa na serikali.
Mmoja
wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Joyce, alisema ni
wazi Serikali ikiandaa utaratibu mzuri wa kuwatambua itawafanya waweze
kulipa kodi ambayo italiongezea pato taifa tofauti na ilivyo sasa ambapo
wamekuwa hawalipi kodi kwa kuwa hawatambuliwi.
"
Sisi kazi yetu ina kipato kizuri kutokana na makubaliano yanayofanyika
kati na wateja wetu lakini Serikali haitaki kututambua hivyo sio rahisi
hata kututaka tulipe kodi, nchi nyingine watu kama sisi tumetambuliwa na
tunalipa kodi serikalini" alisema Rosemary Kazeze.
Aliongeza
kwamba kipindi hiki ambacho Serikali inatafakari au haioni umuhimu wa
wao kutolipa kodi, anawashauri kina dada poa wenzake kuacha tabia ya
kukwepa kwenda Nyumba za kulala wageni zinazotambuliwa na Serikali kwani
kufanya hivyo kunaikosesha serikali mapato
Alisema
kuwa siku za nyuma walikuwa wanafanya biashara hiyo katika madanguro
kitendo ambacho polisi walikuwa wakiwasumbua kwa kuwakamata kutokana na
misako ya mara kwa mara, lakini hivi sasa hawasumbuliwi kwani wamepanga
vyumba katika gesti halali na wanalipia vyumba hivyo na mmiliki analipa
kodi kwa msingi huo nao wanachangia pato la taifa.
“
Kaka yangu mwandishi tunashukuru sana hata wewe kutufikia, wanatudharau
na kutunyanyasa sisi lakini wateja wetu wakubwa ni hao hao viongozi wa
serikali na tasisi nyingine lakini wajue kufanya biashara ya ukahaba sio
sababu ya kuto muunga mkono Rais wetu katika suala la mapato ya
serikali”…alisema Mayasa Hussein
0 comments:
Post a Comment