Real Madrid wameripotiwa kuwapeleka mahakamani klabu ya Benfica juu ya
mauzo ya mchezaji wa kiargentina Ezequiel Garay kwenda Zenit Saint
Petersburg.
Madrid, ambao walimuuuza Garay kwenda Benfica mnamo mwaka 2011,
walikuwa na haki ya kupata 50% ya mauzo yoyote ya mbeleni ya Garay na
wanaamini mauzo yake ya kwenda Zenit yalikuwa chini ya thamani. Ripoti kutoka gazeti la Diario De Noticias kwamba Los Blancos wamegundua kwamba Bayern Munich walitaka kumsajili Garay akiwa Benfica, na waliweka ofa ya €15m mezani, ofa iliyokataliwa na klabu ya Ureno.
Hata hivyo, baada ya muda mfupi, Garay akauzwa kwenda Zenit kwa ada ndogo ya 6 million euros. Benfica walikuwa na haki ya kupata asilimia 40% tu ya mauzo ya mchezaji, asilimia 10 ilikuwa haki ya mmiliki wa 3 – Benfica Stars Fund.
Garay, 29, ambaye aliihama Madrid kama sehemu ya dili la Madrid kumsaini Fabio Coentrao, Garay alijiunga na Madrid akitokea Valencia kwa €20m.
Kesi hii ya Madrid vs Benfica itatolewa maamuzi baadae mwezi huu na mahakama ya michezo duniani – CAS.
0 comments:
Post a Comment