KIKOSI
cha timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens,
kimebeba kombe la Chalenji kwa mara ya kwanza na kuweka rekodi.
Timu
ya taifa ya Tanzania Bara kwa wanawake imewachapa Wakenya kwa maabo 2-1
katika mechi ya fainali iliyochezwa Uganda na kubeba kombe hilo.
Rekodi
yenyewe ni hii, kuwa wao ndiyo timu ya kwanza ya Ukanda wa Afrika
Mashariki kubeba Kombe la Chalenji ambalo limefanyika kwa mara ya
kwanza.
Kilimanjaro
Queens, sawa, lakini kilikosi hicho kwa zaidi ya asilimia 90 ndiyo wale
Twiga Stars ambao ni timu ya taifa ya Tanzania.
Akina dada ambao sasa wanaondoka kwenye sura za utoto, wamekuzwa na kufikishwa hapo na watu wengi sana waliojitolea.
nimeona pongezi nyingi zinakwenda kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ni jambo jema kwa kuwa mwishoni hapa wamejitolea kwa ajili yao.
Lakini
nimeona niwakumbushe wadau kwamba mafanikio ya kikosi hicho, sifa
nyingi ziwaendee waanzilishi wa Sayari FC, waanzilishi wa Mburahati
Queens akiwemo Dk Tamba na wengine walioanzisha timu za wanawake.
Pongezi
zaidi kwa Chama cha Soka Kinondoni (KIfa) ambacho kilionyesha kuthamini
soka la wanawake tokea mwanzo na viongozi wake kama Mchaki, walikuwa
kiwapambana kwa muda mrefu.
Wakati
wa TFF ya Leodeger Tenga, pia walionyesha kuijali timu ya taifa ya
wanawake ambayo wachezaji wake wengi leo ndiyo wamechukua ubingwa huo wa
Afrika Mashariki. Kama unakumbuka walivuka hatua kadhaa za michuano ya
Afrika.
Wako
wadau walijitokeza na kuonyesha upendo wao wa dhati na kuunga mkono
uchezaji wa Twiga Stars na ligi ya wanake. Ninaamini wachezaji wa Twiga
Stars wanaweza kusema mtu kama Dk Damas Ndumbaro alivyokuwa akijitolea
na kuwapa moyo ikiwa ni pamoja na kuwanunulia vifaa wengine.
Twiga
Stars inaing’oa Ethiopia kwao jijini Addis Ababa, Dk Ndumbaro alikuwa
kati ya viongozi wa msafara uliokuwa jijini humo na hata baada ya mechi
vijana walikimbia na kumkumbubatia kwa furaha wakionyesha kuthamini
mchango wake.
Kwa
sasa, Waziri Nape Nnauye ambaye ana dhamana ya michezo, ameonyesha
uzalendo na ushiriki wake kwa karibu tofauti na awali ilivyokuwa kwa
viongozi waliopita.
Huu ni uwakilishi mzuri wa serikali michezoni na unachagiza kwa kiasi kikubwa mafanikio hayo yanayojitokeza kwa sasa pia.
Akina
dada wa Kili Queens, hakika hongera sana kwa kuibandua Kenya na kubeba
Chalenji. Lakini bado mna safari ndefu kuendelea kuusukuma mchezo wa
soka kwa wanawale na ukweli ni kwamba mlichofanya ni kuionyesha jamii
kwamba mnaweza.
Maana yake, wadau wawape nafasi zaidi, wawathamini zaidi na kuwasukuma zaidi muendelee kufanya vema.
Kuna
mtihani kwa Zanzibar, kikosi chao ni dhaifu sana. Huenda changamoto ya
ushindi wenu inaweza kuwa sehemu ya chachu ya wao kubadilika pia kama
watakuwa na hamu ya kubadilika na kupata mafanikio.
Hongera kwa kila mmoja aliyewahi kutoa mchango wake wa aina yoyote kuiunga Twiga Stars. Lakini bado safari haijafikia tamati.
0 comments:
Post a Comment