Kadi za kilektroniki kwa ajili ya kuingia uwanjani zitakuwa zikitolewa bure.
Hii
ni ni baada ya ya hivi karibuni serikali kufunga mashine za
kielektroniki katika Uwanja wa Taifa, kadi kwa ajili ya kuingilia
uwanjani humo zitatolewa bure.
Serikali
iliamua kufunga mashine hizo katika uwanja huo ili kuondokana na mfumo
wa zamani wa kutumia tiketi za kawaida kwa lengo la kulinda mapato yake
uwanjani hapo ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa yakiishia mifukoni mwa
wajanja wachache.
Akizungumza
katika semina elekezi ya jinsi ya kutumia mfumo huo mpya wa kuingia
uwanjani humo uliozinduliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye, Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom ambayo ndiyo
iliyopewa jukumu la kusimamia mfumo huo, Gallus Runyeta amesema kuwa
kadi zitakazokuwa zikitumika katika mfumo huo zitatolewa bure.
Amesema
kadi hizo zitaanza kutolewa hivi karibuni ambapo kutakuwa na mchezo wa
Ligi Kuu Bara utakaofanyika katika uwanja huo ambao serikali kwa
kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) watauandaa kabla ya
mchezo wa Yanga na Simba.
“Kadi
zinapatikana kwa mawakala wetu (wa Selcom) waliopo kila sehemu. Lazima
ununue tiketi halafu unapewa kadi bure,” alisema Runyeta.
Akizungumzia
jinsi ya kuitumia kadi hiyo, Runyeta amesema: “Utajisajili kwa kupiga
*150*50# halafu ni lazima uiwekee pesa kwa Airtel au M-Pesa. Kiwango cha
chini cha kuongeza salio ni Sh 1,000.
“Unaweza
ukanunua mechi moja kwa kuandika tarehe na mchezo husika au ukachagua
baadhi ya mechi au ukanunua mechi zote za msimu za timu unayoipenda.
“Unapokwenda
kuingia uwanjani, utaweka kadi yako kwenye alama husika na mlango
utafunguka wenyewe. Ukishaangalia mechi uliyoinunua, hauwezi kesho yake
ukaenda kutazama mechi nyingine ambayo hujailipia. Kadi itasoma kwenye
mechi zilizolipiwa tu. Ukiingia uwanjani hauwezi ukatoka halafu ukarudi
kwa tiketi ileile.
Tunawashauri
watu wawe wananunua tiketi mapema ili kuepusha usumbufu na msongamano
milangoni. Unaweza ukanunua siku nyingi kabla.”
Ameongeza:
“Mbali na kadi hizo kuzitumia uwanjani, pia aliyenayo anaweza kuitumia
kwa matumizi mengine kama vile kuhifadhi na kutoa fedha kwa wakala,
lakini pia inamwezesha mtu huyo kulipia bidhaa na huduma mbalimbali bila
kuwa na fedha mfukoni.”
Wakati
huohuo, Nnauye amemuagiza Naibu Mkurugenzi wa Michezo Tanzania,
Nkenyenge Alex kuhakikisha anaandaa sera ya michezo nchini mapema
iwezekanavyo mpaka kufikia mwezi Septemba iwe tayari.
Amesema
lengo kubwa la kufanya hivyo ni kutaka kuleta mapinduzi makubwa ya
michezo hapa nchini kwani sera iliyopo hivi sasa imeshapitwa na wakati.
“Nimemwambia
nataka mpaka kufikia Septemba sera hiyo iwe tayari, kama atashindwa
kufanya hivyo, basi akatafute sehemu nyingine ya kufanya kazi pamoja na
wenzake wote,” amesema Nnauye.
0 comments:
Post a Comment