Baada ya simu mpya za kampuni ya Apple,
aina ya iPhone 7s kuingia sokoni kwa mara ya kwanza mwishoni mwa juma
lililopita, watu wengi walionekana wakijipanga misururu katika maduka ya
kampuni hiyo katika nchi tofauti ili kununua simu hizo.
Nchini China hali ilikuwa vivyo hivyo, lakini kukiwa pia na visa vya watu wakitaka kuziiba Hong Kong.
Lakini licha ya wote waliokuwa
wakihangaika kujitahidi kuwa wa kwanza kuipata simu hiyo, mbwa mmoja
(Coco) yeye alikuwa ametulia.
Mmiliki wa mbwa huyo, Wang Sicong, ambaye
ni mtoto wa bilionea wa Kichina, Wang Juanlin (mwenye utajiri wa
takribani dola bilioni 30) alimnunulia mbwa wake simu 8 aina ya iPhone
7s siku zilipowasili nchini China kwa mara ya kwanza.
Watu mbalimbali walikuwa na maoni tofauti katika mtandao wa Weibo huko Uchina kuhusu jambo hilo.
Hii si mara ya kwanza kumnunulia mbwa huyo
vitu vya thamani kwani aliwahi kumvalisha saa bili za Apple zenye
thamani ya dola elfu 37,000 (Zaidi ya shilingi milioni 70 za Kitanzania).
Wang amekuwa akifanya vioja mbalimbali na mbwa wake huyo kwa kutumia
utajiri wa baba yake ambao wakati mwingine wananchi wa China huchukizwa
na matendo yake na kuandika maneno ya kumkashifu kwenye mitandao ya
kijamii.
0 comments:
Post a Comment