Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>WABUNGE WA UKAWA WAANZA MAKEKE BUNGENI.FAHAMU ZAIDI HAPA.
SIKU moja baada ya wabunge wa Kambi ya
Upinzani Bungeni kurejea katika chombo hicho cha kutunga sheria,
wameibua msuguano na wenzao baada ya michango yao katika Muswada wa
Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa wa Mwaka 2016, kutofautiana na wenzao
wengi.
Wanadai kuwa muswada huo hauna maslahi
kwa Taifa, bali unalenga kukandamiza uhuru wa kupata habari kama
ulivyoainishwa katika Ibara ya 18 (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania.
Wabunge wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Godbless Lema (Arusha Mjini), Pauline Gekul (Babati
Mjini), David Silinde (Momba), Peter Msigwa (Iringa Mjini), Kasuku
Bilago (Buyungu) na Mwita Mwikwabe (Ukonga) walioushambulia muswada huo,
wakisema una lengo la kuzuia vyombo vya habari visifanye kazi.
Kwa nyakati tofauti, wabunge hao
walitofautiana na Muswada huo wakisema hauna maslahi kwa taifa, bali
unalenga kukandamiza uhuru wa kupata habari kama unavyoanishiwa katika
Ibara ya 18 (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayosema
“Kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio
mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu
masuala muhimu kwa jamii.”
Baada ya wabunge wengi waliochangia
muswada huo tangu asubuhi kupongeza, Lema alilalamikia muswada huo huku
akisema sheria zitawahukumu watu wanaoushabikia muswada huo.
“Kwa wingi wenu mtafanikiwa kuupitisha
muswada huu, lakini muswada huu hauna jipya zaidi ya kutaka kuvidhibiti
vyombo vya habari ambavyo vinapokea taarifa nyingi sana…vyombo vya
habari vikiminywa, sisi wabunge wa upinzani tukiminywa, unadhani
kutakuwa na nini hapa? Hakika mshahara wa dhambi daima ni mauti,”
alisema.
0 comments:
Post a Comment