Baada
ya kupona majeraha ya nyonga, beki wa kulia wa Klabu Bingwa ya Afrika
Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe, amesema kuwa hivi sasa
anapambana vilivyo kurejesha makali yake yaliyomfanya akubalike na
mashabiki wa timu hiyo.
Beki
huyo kipenzi wa mashabiki wengi wa soka nchini, amerejea mazoezini hivi
sasa kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara
(VPL), alishindwa kuitumikia vema timu hiyo baada ya kukosa mechi 10 za
mwisho za mzunguko wa kwanza wa ligi kufuatia majeraha hayo.
Akizungumza
na mtandao rasmi wa klabu hiyo Kapombe alisema kuwa kwa sasa anazidi
kujiandaa vema kupitia mazoezi wanayopewa na benchi la ufundi la timu
hiyo pamoja na mengine binafsi anayoyafanya peke yake.
“Mimi
binafsi nimejiandaa vizuri na naendelea kujiandaa vizuri kwa mazoezi
ambayo tunapewa na mengine ya kwangu binafsi, yote hayo nafanya ili
kupambana na kurejesha makali yangu ili kuisaidia Azam FC,” alisema.
Kapombe
alisema kwa sasa anaendelea vizuri na afya yake ipo vizuri kabisa
kuweza kupambana kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mzunguko wa pili wa
ligi unaoanza Jumamosi ya wikiendi hii.
Sura mpya dirisha dogo
Kapombe
pia alifurahishwa na namna wachezaji wapya waliosajiliwa kwenye dirisha
dogo la usajili, ambapo amedai kuwa ni wachezaji wazuri na anaamini ya
kuwa wataisadia sana Azam FC kuelekea mechi za mzunguko wa pili.
“Mpaka
sasa kuna sura mpya ambazo zimeongezwa, ni wachezaji wazuri wanaokuja
kuziba mapungufu ambayo tumayaona mzunguko wa kwanza, kila mchezaji
aliyekuja hapa anasifa yake na uzuri wake kuweza kuisaidia timu yetu
katika kufikia malengo tuliyojiwekea,” alisema.
Hajawaacha mashabiki
Beki
huyo mwenye sifa ya kupandisha mashambulizi kwa kasi na uwezo kufunga
mabao, aliyeweka nyavuni mabao 11 msimu uliopita, kuelekea raundi ya
pili ya ligi amewaachia ujumbe mashabiki wa timu hiyo akiwaambia kuwa
waunganishe nguvu kuwasapoti uwanjani katika mechi zao.
“Mimi
ninachowaomba mashabiki wa Azam FC ni waendelee kuwa nasi katika vipindi
vyote vya shida na raha, waunganishe nguvu na waendelee kutusapoti
katika mechi za raundi ya pili ili na sisi tuweze kufika pale Azam FC
inapohitajika kufika,” alimalizia.
Azam
FC inayodhaminiwa na kinywaji safi cha Azam Cola, kinachoburudisha koo
na kuchangamsha mwili pamoja na Benki bora kwa usalama wa fedha zako ya
NMB, inatarajia kufungua ng’we ya mzunguko wa pili kwa kukipiga na
African Lyon Jumapili hii Desemba 18 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es
Salaam saa 10.00 jioni.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment