Rais Magufuli leo wakati akizindua majengo ya Hostel za Chuo Kikuu
Cha Dar es Salaam (UDSM) amefunguka na kusema sasa anasubiri ripoti ya
wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wanatumia vyeti vya
kufoji.
Rais Magufuli amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kila
sekta hivyo sasa anasubiri hiyo ripoti ili aweze kuifanyika kazi na
kutenda haki katika jambo hilo.
“Naisubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa
ambao wana vyeti vya kufoji ili niifanyie kazi” alisema Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli ameitaka Taasisi ya TCU kuacha
kuwapangia wanafunzi vyuo bali wanafunzi wanapaswa kuwa huru kuchagua
aina ya vyuo ambavyo wao wanataka kwenda na kusema kwa kufanya hivyo
itatoa nafasi kila chuo kuwa na wanafunzi wa kutosha huku wanafunzi pia
wakienda kusoma sehemu ambazo wao wanahitaji kwenda kusoma na si
kuwapangia.
“Mtu amefaulu ana sifa zake anataka kuja kusoma Chuo Kikuu Cha Dar
es Salaam afaidi mabweni ya Magufuli analazimishwa kupelekwa kwenye ka
chuo ambako wala hakana jina hata ukitafuta kwenye mtandao hakaonekani,
akasome pale wakati hawana hata mabweni na saa zingine hata walimu
hawana, tunawatesa watoto hawa na saa zingine wakuu wa vyo vile wamekuwa
na tabia ya kwenda kwenye uongozi wa TCU ingawa sina ushahidi wapangiwe
idadi wa wanafunzi wanaowataka kwenye vyo hivyo, sifahamu wanapangiwa
kwa rushwa lakini wapo pia kuna ushahidi na baadhi ya viongozi wa vyuo
fulani fulani waliofunga safari kwenda TCU kwa ajili ya kuomba wapangiwe
wanafunzi au kutoa shukrani, au hata kwenda kuwasalimu tu” alisema Rais
Magufuli
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment