Mwezi wa Enceladus ambao uko kwenye sayari ya Saturn huenda ukawa mahali bora zaidi pa kwenda kutafuta maisha nje ya dunia.
Tathmini hii inatokea kufuatia uchunguzi katika sayari hiyo yenye kilomita 500 uliofanywa na Cassini.
Uchambuzi wa kemia wa Cassini unaonyesha matundu ya maji moto kwenye
sakafu ya bahari ya Enceladus, maeneo ambayo yanahusishwa na kuwepo kwa
maisha, hapa duniani.
Kuwepo kwa maji haya sio thibitisho kamili kwamba vitu vilivyo na uhai
vinaishi katika mwezi huo mdogo lakini teknolojia zinaweza kutumika
kupima maji hayo na kutoa ushahidi zaidi.
"Tuna uhakika kuwa kitu chenye uhai kinaweza kuishi kwenye bahari ya
Enceladus lakini lazima tufanye utafiti zaidi," alisema mwanasayansi wa
Cassini kutoka Taasisi ya Utafiti ya Southwest, San Antonio, Dkt. Hunter
Waite.
"Iwapo hakuna maisha huko, ni sawa, lakini ikiwa maisha yapo itakuwa bora zaidi," alieleza BBC.
Bahari iliyopo kwenye Enceladus inakisiwa kuwa na kina kirefusana sana
na yapo majimaji kwa sababu ya joto linalotokana na mvuto wa mara kwa
mara kutoka kwenye sayari ya Saturn.
Cassini tayari amedhibitisha kwamba maji hayo yanashikana na sakafu ya
bahari kutokana na aina ya chumvi na silika ambayo pia imeonekana katika
mashimo.
Lakini wanachotaka kujua sana wanasayansi ni ikiwa maswala fulani
yanayotendeka duniani pia yanaweza kufanyika katika Enceladus - kitu
kinachoitwa serpentinisation, ambayo hutengeneza gesi ya hidrojeni.
"Kwa viumbe hai, hidrojeni huwa ni kama kama pipi - ni chakula
wanachokienzi," alieleza Dkt Chris McKay, mwanabiolojia wa maswala ya
anga wa shirika la Nasa.
"Ni nzuri sana kwa kuvipa nguvu, na inaweza kusaidia viumbe vidogo sana.
Kupata hidrojeni itakuwa vizuri sana na itakuwa moja ya ushahidi
utakaoonyesha uwezekano wa kuwepo na uhai."
Viumbe hai anavyozungumzia Dkt McKay vinaitwa methanojeni kwa sababu
vinatengeneza gesi ya metheni vinapogusana na hidrojeni na gesi ya
kaboni .
Nasa, ambayo inaongoza ujumbe wa Cassini , ilitakikana kufanya tangazo
la hidrojeni miezi michache baada ya uchunguzi wa mwisho waroketi ya
mwezini, Oktoba mwaka wa 2015.
Ziara ya Cassini sasa inakamilika . Baada ya kuizunguka Saturn kwa muda
wa miaka 12, inaendelea kuishiwa na mafuta na sasa itawachiliwa kuingia
kwenye anga ya dunia hiyo ya Saturn mwezi Septemba, kuhakikisha kuwa
haiwezi kugongana na Enceladus na kusababisha kuchafuka kwake.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment