Saturday 15 April 2017

Ushauri wa Bill Nass kwa Roma Mkatoliki na wenzake.Fahamu zaidi hapa.

Kupitia kipindi cha The Weekend Chart Show April 14, 2017 kinachorushwa na Clouds TV rapa Bill Nass ambaye anatamba na hit song ya Mazoea amemuasa Roma Mkatoliki na wenzie ambao walikumbwa na mkasa wa kutekwa.

Bill Nass amewataka Roma na wenzie kuendelea na maisha kwa kufanya kazi ingawa hawatokuwa vizuri lakini kwa sababu wana uhai na uzima katika maisha yao wanapaswa kumshukuru Mungu.



”Wanapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwa wako hai. Wendelee kufanya kazi kwa moyo, japo unapokuwa na pressure huwezi kufanya. Kwa mfano, mimi tu nikiwa hivyo mood za studio zinakata. Japo wao wanaweza kuwa zaidi ya hapo, ila hizo ni changamoto tu, so, isiwafanye wakaishia hapo as long as wako hai na wazima.” – Billnass.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment