Tume ya Uchumi na Makosa ya Kifedha (EFCC) nchini Nigeria, jana usiku
ilikamata mabilioni ya fedha za kigeni na fedha za nchi hiyo katika
jumba la kifahari la mwanasiasa mmoja.
Maafisa wa tume hiyo walifika kwa kushtukiza katika jumba hilo baada ya
kupewa taarifa na ‘Msamalia mwema’ na kunasa zaidi ya $38 milioni,
£27,000 na N23 milioni katika jumba hilo lililoko eneo la Ikoyi jijini
Lagos.
Waziri wa Habari na Utamaduni wa nchi hiyo, Alhaji Lai Mohammed alisema
kuwa mtoa taarifa zilizopelekea kukamatwa kwa mabilioni hayo ya fedha
atapewa asilimia tano ya kiasi kilichopatikana.
Serikali ya nchi hiyo hivi karibuni ilieleza faida za watoa taarifa (whistleblowers) na kuahidi kuwa itawalinda.
Serikali ya Nigeria imeeleza kuwa mtoa taarifa zitakazopelekea
kupatikana kwa fedha kuanzia Naira bilioni 5, atapata gawio la Naira
milioni 210 huku ikiweka wazi jinsi ya kukotoa magawio mengine ya mtoa
taarifa kulingana na kiasi cha fedha zitakazokamatwa.
“Kwa mfano, mtoa taarifa akitoa taarifa zitakazopelekea kubainika fedha
zilizofichwa kiasi cha Naira bilioni 10, atapata asilimia tano ya Naira
bilioni 1 za kwanza, na asilimia nne ya Naira bilioni 4 pamoja na
asilimia 2.5 ya Naira bilioni 5 zilizobaki,” Waziri Mohammed anakaririwa
na mtandao wa Vanguardngr.
Serikali ya Nigeria inaendesha oparesheni ya kukamata mabilioni
yaliyofichwa na watu binafsi majumbani kwa lengo la kuyatakatisha
kutokana na biashara haramu na ufisadi, ambapo kabla ya tukio la jana,
tume husika ilikamata mabilioni ya fedha za kigeni kwa mmoja kati ya
wamiliki maarufu wa maduka ya kubadilishia fedha jijini Lagos.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment