Rapa na mtangazaji mkongwe nchini Tanzania Soggy Doggy amefunguka
sababu zilizomfanya akae kando kwenye ramani ya muziki wa hip hop kwa
muda mrefu.
Soggy Doggy
Amesema
ushindani uliopo kwenye soko la muziki na gharama za ufanyaji wa video
zimekuwa ni kubwa, kitu ambacho ni kigumu kukimudu hasa kwa mtu mwenye
majukumu kama yeye.
Soggy amezungumza hayo na kusema muziki
unahitaji matumizi makubwa ya pesa kitu ambacho kilimfanya arudie kazi
yake ya utangazaji lakini hata kama akitaka kurudi kwenye 'game' lazima
arudi kama vijana wa sasa ili muziki wake uonekane bora.
"Nisidanganye kwamba
utangazaji ndiyo uliniachisha kuimba, si kweli maisha mengine ya
kifamilia ndiyo yalinifanya niache muziki. Muziki wa sasa unahitaji
kuwekeza mpaka milioni kumi kwenye video tofauti na zamani ilikuwa laki
tatu tu unapata kichupa. maisha yanabadilika kipindi nataka kutoa
milioni hizo kwenye video moja mwanangu wa kwanza anatakiwa aingie
kidato cha kwanza ndiyo maana nikaamua kuacha kwanza muziki niangalie
mambo mengine ya kifamilia. Nafurahi sana Jay Moe alivyopokelewa na hata
siku mimi nikirudi kwenye game sitarudi kizembe lazima kwanza
nijipange" Alisema Soggy.
Hata hivyo Soggy amewashauri vijana wa
sasa wanaofanya muziki kutumia muda mrefu kwenye kuandika na kuhariri
mashairi yao ili kuepuka adha za kufungiwa kazi zao na vyombo husika.
Chanzo:Eatv
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment