Idara ya Uhamiaji nchini Tanzania imetoa siku 90 kwa wageni kufanya
uhakiki wa vibali vya ukaazi ili kuimarisha udhibiti wa wageni wanaoishi
nchini pamoja na kuzuia mianya ya upotevu wa maduhuli ya serikali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna
Makakala baada ya uzinduzi wa mfumo wa uhakiki kwa kutumia njia ya
kielekroniki amesema mfumo huo ni rahisi na unatoa fursa kwa waajiri na
wageni wote wenye vibali vya ukaazi kuhakiki kumbukumbu za vibali vyao
ili kujua kama vimetolewa na mamlaka husika.
Dkt. Makakala amezitaka taasisi na mashirika binafsi baada ya kuhakiki
vibali vya wageni wao watatakiwa kuwasilisha taarifa za vibali hivyo
katika ofisi za Idara ya Uhamiaji za mikoa zilizopo karibu na ofisi hizo
ambapo amesema baada ya muda huo kuisha wale wote ambao hawajahakiki
hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment