Tuesday 30 June 2015

BREAKING NEWS:Kutoka Indonesia ndege ya kijeshi yaua watu 30.





Maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege ya uchukuzi ya jeshi la angani la nchi hiyo imeanguka kaskazini mwa jimbo la Sumatra.
Wanasema kuwa tayari miili 20 zimepatikana katika eneo la ajali.
Maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege hiyo ya uchukuzi ya majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.
Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya Hercules ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 50 ilipoanguka.

0 comments:

Post a Comment