Tuesday 30 June 2015

ZITO KABWE:Serikali ya Muungano inatunga Sheria mpya za jambo la Muungano litalohitaji kuridhiwa na Baraza la Wawakilishi.




HIKI NDICHO ALICHOKISEMA ZITO KABWE KWENYE UKULASA WAKE WA TWITTER.
Serikali ya Muungano inatunga Sheria mpya za jambo la Muungano litalohitaji kuridhiwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati Baraza limeshavunjwa.
- Sheria ya Mafuta na Gesi Asilia ya mwaka 2015
- Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi ya mwaka 2015
Muswada wa Petroli wa mwaka 2015 unaunda upya TPDC ambayo uanzishwaji wake ( Establishment Order ) ulikuwa ni wa Tanzania Bara tu. Muswada unataka TPDC itumike Bara na Zanzibar kisheria.
Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi unataka fedha zote za Mafuta na Gesi ziingie Hazina ya Muungano hata kama Mafuta hayo yapo Zanzibar.
CCM inawachezea shere Wazanzibar


0 comments:

Post a Comment