Monday 29 June 2015

HABARI MOTO:Zanzibar mwandishi wa Habari apigwa na kuumiza vibaya na Polisi, alikuwa akichukua Habari katika kituo cha Uandikishaji wapiga kura.




Mwandishi wa Habari kwa jina Omar Ali mzaliwa wa Mkoani Kangani kisiwani Pemba, jana mida ya asubuhi ameshambuliwa na kupigwa vibaya sana na jeshi la Polisi Zanzibar na kutupwa maeneo ya Maisara mjini Zanzibar.

Mwandishi huyu alikuwa anachukua habari kutoka kituo cha uandikishaji dafatari la kudumu maeneo ya Migombani Zanzibar na polisi hao inasadikiwa walisema ni mwandishi wa Chama cha Wananchi CUF na ndipo walipomshika na kuanza kumpiga vibaya sana na kumvunja miguu kama anavyoonekana kwenye picha akiwa hospital mahutui miguu ikiwa imevujika.

0 comments:

Post a Comment