TUREJEE KWENYE KAMUSI KUTAFUTA MAANA YA NENO RAIS NA RAHISI KABLA
YA KUTANGAZA NIA
Habari ya wewe ndugu yangu popote ulipo ni matumaini yangu kuwa hu
mzima wa afya na unaendelea vyema na majukumu yako katika ujenzi wa taifa, leo
nimewiwa kuzungumzia mada yenye kichwa habari tajwa hapo juu kwa kuwa nimeona
idadi inayovuta hisia za watu wengi kwenye suala la watangaza nia wa chama
chetu tawala CCM. Unaweza kujiuliza mpaka inafika idadi kubwa ya watu kwa kiasi
kile ni utashi wa kisiasa,kukua kwa kidemokrasia,kuona ikulu ni patamu kama
ndizi kisukari au mithili ya asali napata shida kuelewa jambo hili kwani bado
najiuliza hawa watangaza nia wote wanazani kupewa ridhaa ya kuwa RAIS ni RAHISI
au wanajua wanachokifanya??
Mimi binafsi
nimewahi shuhudia demokrasia ya kweli darasani wakati wa kumchagua kiongozi wa
darasa wale wenzangu wa st. kayumba tulikuwa tukiwaita monitors/monitress
(kiranja) pamoja na kuhisi kuwa hii ni ngazi ya chini kabisa kujifunza uongozi
au kuonesha kuwa wewe ni kiongozi wa badae sijawahi kuona wagombea hata
ukiranja wakifika kumi katika darasa labda walikuwa wakiofia ni nani atapiga
kula kama wote tutaamua kuwa wagombea.
Agenda zangu
binafsi au maswali ninayojiuliza kutokana na watangaza nia kuwa utitiri (wengi
kupita kiasi)
1.
Ina maana wote hawa hakuna mwenye
imani na mwenzake kuwa ni kiongozi anayestahili, sikiliza hotuba zao utanielewa
tu, kila mtu anasema nitafanya hiki nitafanya kile sio kama huyu wala sio kama
yule kwani yule na yule pale ni mafisadi au sababu wanazozijua wao binafsi.
2.
Au ndio maandalizi ya goli la
mkono kama alivyosema kiongozi wetu katibu wa itikadi na uenezi ili mradi tu
refa asione? Naanza kujiuliza haya kwakuwa hawachelewi kutuletea hesabu za
sayari ya tano(jupiter) watangaza nia 40 wakitimiza masharti ya kuwa na wadhamini
nchi nzima kwa kila mkoa na kila mmoja kufikisha idadi tajwa ya wadhamini
ukizisha mara 40 mara mikoa yote unaweza pata mtaji mzuri wa kula ambazo wazee
wa goli la mkono wanaweza kutuambia ni mtaji wao wa kuanzia kama kura wenye
uhakika nazo kwani leo hii mtu awezi kuidhamini yanga tena akiwa mwanachama hai
wa yanga alafu akashangilia simba sijui kama tunaelewana wandugu.
3.
Hivi walimu walio kuwa
wakitufundisha methali,nahau,vitendawili,misemo na maneno mengi ya busara kama
FIKIRI KABLA YA KUTENDA walikuwa hawajawahi kuwafundisha hawa wenzetu au mimi
nitakuwa nimepanic?? Kama mtu unaweza fikiri kabla ya kutenda ni bora
ukajipima,ukapima na upande wa pili na kukubali matokeo kwani nafikiri wapo
wengi tu katika kundi la watu 40 ambao wanajua fika kabisa kuwa kutaka ridhaa
ya URAIS si RAHISI na wanajua kabisa kuwa sifa,vigezo na hata mvuto wa kisiasa
hawana ila wamekazana na kuchukua fomu.
Tutaendelea
tena kesho Mungu akipenda, nchi yangu bado changa wacha nijikongoje kwenda
kuijenga nchi mie, wengine watakuja kupaka rangi wakishamaliza kutuletea
maigizo na kutufanya kama watoto. Uwazari tu ulikuwa changamoto sasa ili la
URAIS sijui wanalichukuliaje???
0 comments:
Post a Comment